WHO: Tanzania haikutoa taarifa kuhusu ugonjwa wa Ebola

Nipashe Online: Shirika la afya duniani limelalamikia ukosefu wa ushirikiano kutoka serikali ya Tanzania katika utoaji taarifa kuhusu visa vinavyoshukiwa kuwa vya Ebola nchini.

Katika taarifa yake ya malalamiko, shiriki hilo limeeleza kwamba uwazi na kasi katika kukabiliana na virusi vya ugonjwa huo hatari ni muhimu katika kudhibiti mlipuko ambao tayari umetajwa kuwa janga la afya duniani.

Katika taarifa hiyo iliyotolewa Jumamosi, WHO limeeleza kwamba kufuatia taarifa zisizokuwa rasmi kuhusu visa vya ugonjwa na jitihada zake kupata taarifa kutoka kwa idara husika Tanzania kuhusu hali nchini humo, mpaka sasa hawajapokea data za kliniki, matokeo ya uchunguzi, mawasiliano na watu husika na hata matokeo ya uchunguzi wa maabara waliofanyiwa wagonjwa hao wanaoshukiwa.

Kufikia sasa jitihada zetu za kuifikia serikali ya Tanzania kutoa tamko kuhusu taarifa hii ya WHO hazijafuwa dafu.

WHO lilituma kundi la wataalamu kuchunguza kisa cha ugonjwa usiojulikana na ubalozi wa Marekani ulifuatilia hatua hiyo kwa kutoa tahadhari.

Hatua hiyo ilisababisha uvumi katika mitandao ya kijamii kwamba ugonjwa huo hatari umeingia nchini Tanzania.

Waziri wa afya Tanzania Ummy MwalimuHaki miliki ya picha@UMWALIMU-Waziri wa afya Tanzania Ummy Mwalimu wiki iliyopita amesena hakuna kisa hata kimoja cha ebola katika taifa hilo.

Serikali ya Tanzania imesema nini?

Serikali ya Tanzania ilifutilia mbali uvumi kwamba kuna visa vya ugonjwa wa Ebola nchini humo.

Waziri wa afya nchini humo bi Ummy Mwalimu aliambia mkutano na wanahabari kwamba hakuna kisa hata kimoja cha ebola katika taifa hilo.

Alisema kwamba taifa hilo limejiandaa kukabiliana na mlipuko wowote wa ugonjwa na tayari limefanya majarabio ili kujua jinsi ilivyojiandaa huku ikiweka tayari vituo vya kuwatenga waathiriwa.

Shirika hilo la Umoja wa mataifa limeendelea kueleza katika taarifa yake kwamba lilifahamishwa mnamo Septemba 10 kuhusu kifo cha mgonjwa kilichotokea mjinia dar es salaam, na kuarifiwa kwa njia isiyo rasmi siku ya pili kwamba mgonjwa huyo alipatikana kuwa na Ebola baada ya kufanyiwa vipimo.

Kadhalika WHO linaeleza kwamba liliarifiwa kuhusu visa vingine viwili vinavyoshukiwa kuwa vya ugonjwa wa Ebola nchini humo.

Mmoja kati yao, alikutikana kutokuwa na Ebola baada ya vipimo na hapakuwa na taarifa zozote kuhusu mgonjwa wa pili, imeeleza taarifa hiyo.

ebolaHaki miliki ya picha WIZARA YA AFYA TANZANIA

”Nataka kuwahakikishia kwamba idara ya afya ilichukua sampuli na matokeo yake ni kwamba wawili hao hawakuwa na ugonjwa wa Ebola. Hakuna Ebola Tanzania na watu hawafai kuwa na wasiwasi”, alisema waziri wa afya Tanzania Ummy Mwalimu wiki iliyopita kuhusu uvumi wa visa hivyo.

Kufanya vipimo tena vya homa ya Ebola katika maabara inashauriwa sana ili kuthibitisha matokeo ya vipimo na hivyo kubaini aina ya virusi Ebola . WHO linasema kuwa limewapatia maafisa wa Tanzania ushauri huu.

Mgonjwa huyo ambaye inaarifiwa ni mwanamke alifariki tarehe 8 Septemba kwa mujibu wa WHO.

Msururu wa matukio ya mgonjwa aliyeshukiwa kuwa na Ebola

Tarehe 10 Septemba 2019, Shrika la Afya duniani WHO lilipokea ripoti ya taarifa ya kisa cha mambukizi ya Ebola mjini Dar es Salaam, Tanzania.

Kisa hicho kinachoshukiwa kilimhusu mwanamke mwenye umri wa miaka 34 ambaye alikuwa akisomea nchini Uganda.

Aliwasili nchini Uganda akitokea nchini Tanzania tarehe 08 Agosti 2019.

Taarifa hiyo inasema kwa kuanzia tarehe 08 hadi 22 Agosti, alikuwa katika eneo la kati la Uganda, akiishi katika hosteli ya kibinafsi karibu na mji mkuu Kampala.

Ebola ni nini?

The Ebola virusHaki miliki ya picha BSIP/GETTY IMAGES

Ebola ni kirusi ambacho mwanzo husababisha joto la mwili na kudhoofisha misuli na uvimbe kooni.

Kisha mgojwa huanza kutapika, kuharisha na kuvuja damu ndani na hata nje ya mwili.

Watu huambukizwa wanapogusana moja kwa moja kupitia michubuko ya mwili, au mdomo na pua, huku damu, matapishi, kinyesi au kugusa majimaji ya mwili ya mgonjwawa Ebola

Wagonjwa huwa wanakufa kutokana na ukosefu wa maji mwilini na kuharibika kwa viungo vya ndani vya mwili.