Watu wanaokunywa kahawa wanaishi miaka mingi: Utafiti

Ukikunywa vikombe vitatu vya kahawa kwa siku unaweza kuishi miaka mingi, kwa mujibu wa utafiti uliofanyiwa karibu watu nusu milioni kutoka nchi 10 za Ulaya.

Utafiti huo uliochapishwa kwenye jarida na Annals of Internal Medicine, unasema kuwa unywaji wa kahawa unaweza kuongeza maisha ya mtu.

Lakini wataalamau wanasema kuwa ni vigumu kusema kuwa ikiwa ni unywaji kahawa unachangia watu kuishi miaka mingi au ni maisha ya kiafya wanayoishi wanywaji kahawa.

Watafiti kutoka shirika la Agency for Research on Cancer and Imperial College London, wanasema wamegundua kuwa unywaji wa kahawa nyingi unahusiana na hatari kidogo ya kufariki hasa kutokana na magonjwa ya moyo.

Waliafikia uamuzi baada ya kuchunguza takwimu kutoka kwa watu walio na umri wa zaidi ya miaka 35 kutoka nchi 10 za Ulaya

Waliawauliza watu wakati wakianza utafiti kuhusu kiasi cha kahawa walikuwa wakinywa kisha wakaangali vifo vilivyotokea katika kipindi cha miaka 16.

Lakini cha kuvunja moyo kwa wanywaji wa kahawa, ni kuwa ugunduzi huu haueleweki vyema.