Wanawake ambao watazaa watoto wanne hawatalipa kodi nchini Hungary

Wanawake ambao watazaa watoto wanne na zaidi nchini Hungary hawatalipa kodi maishani mwao, kwa mujibu wa waziri mkuu wa nchi hiyo, wakati akizindua mipango ya kuongeza idadi ya watoto wanaozaliwa nchini humo.

Hii ni njia ya kulinda hatma ya nchi bila kutegemea wahamiaji. alisema Viktor Orban.

Mwanasiasa huyo wa mrengo wa kulia anapinga uhamiaji hasa kutoka kwa waislamu.

Idadi ya watu nchini Hungarry inashuka kwa watu 32,000 kwa mwaka na wanawake wana watoto wachache kuliko makadirio mengine ya nchi za EU.

Kama sehemu ya hatua, wanandoa wachanga watapewa mikopo isiyo na riba ya hadi dola 36,000.

Bw Orban alisema kwa nchi za Magharibi, jibu la kushuka kwa watoto wanaozaliwa barani Ulaya ni uhamiaji, kwa kila mtoto ambaye hayuko mwingine atakuwa njiani na idadi itakuwa sawa.

“Kwa watu wa Hungary fikra ni tofauti,” alisema. Hatutaki idadi. Tunataka watoto wa Hungary.”