Wanasayansi wagundua chumvi inayowezi kutumika katika chakula mwezini

Nipashe Online: Bahari kubwa inayopatikana katika mwezi wa sayari ya Jupiter ina chumvi- kama ile inayotumia katika samaki wako na viazi karai!

Kulingana na wanasayansi, darubini ya Hubble imekuwa ikichunguza mwezi kwa Jina Europa kwa muda mrefu sasa na imepata chumvi kama ile inayotumiwa katika chakula.

Chumvi inayotumika katika chakula ndio inayozifanya bahari kuwa chumvi.

Watafiti wanasema inamaanisha kwamba bahari inakabiliwa na vitendo vya Volakano.

Inafurahisha kwa sababu inaongeza fursa ya kuwepo kwa ishara za maisha ya ziada katika mwezi.

Duniani maisha husemekana kuanzia eneo la chini la bahari lenye maji yanayochemka.

Shirika la anga za juu nchini Marekani Nasa linakaribia kuanza uchunguzi mwezini- huku ujumbe wa kwanza ukitarajiwa kuondoka 2023.

Hadi kufikia wakati huo, wakati pekee ambao wanasayansi wameuona mwezi kwa karibu ni mwisho wa miaka ya 90 na mapema mwaka 2000 kupitia ndege kwa jina Galileo.

Rangi ya njano inayopatilkana katika mwezi ni chumvi inayotumika katika chakula
Kwa kutumia mwanga wa Infrared, wanasayansi walitafuta vipengee mbalimbali.

Chumvi hiyo ilipatikana hususan karibu na barafu na safu ya milima inayopita katika sakafu yake.

Profesa Mike Brown , kutoka Taasisi ya teknolojia ya California, alisema: Tumekuwa na uwezo kufanya tathimini na darubini kwa takriban miaka 20. ”Ni kitu ambacho hakuna aliyefikiria kufanya”.

Pengine katika siku zijazo utakuwa ukitumia chumvi inayotoka ulimwengu mwengine.