Wanamuziki Watano Matajiri Zaidi Duniani

Jay-Z

Jay Z: Dola milioni 900 

Utajiri wa Jay Z uliongezeka kutoka dola, milioni 810 hadi dola milioni 900 katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita na kumwezesha kushikilia nafasi ya kwanza ya wanamuziki matajiri kwa mara ya kwanza kabisa tangu jarida la Forbes lianze kuwaorodhesha wanamuziki matajiri duniani.

Kuongezeka kwa utajiri wale kulitokana haswa na kupanda kwa thamani ya bidhaa zake za pombe za Armand de Brignac na D’Usse’ cognac, huku lebo yake ya muziki ya Roc Nation na Tidal zikichangia asilimia kidogo katika utajiri wake.

P. Diddy: Dola milioni 825 

P DIDDY

P Diddy alishuka kutoka nafasi ya kwanza baada ya kuishikilia tangu mwaka 2011. Utajiri wake umekuwa ukiongezeka mwaka uliopita licha ya kutotoa albamu lakini mapato yake hayakuwa ya kutosha kumwezesha aendelee kushukilia nafasi ya kwanza.

Kupungua kwa soko la mvinyo wa vodka kumeathiri mapato yake sawa na kwenye sekta ya televisheni ambapo ana hisa. Lakini kampuni yake ya DeLeón tequila imekuwa nguzo yake kuu ya kuongezeka kwa utajiri wake.

Dr Dre: Dola milioni 770 

Dr DRE

Produsa huyu amekuwa kwenye orodha hii tangu mwaka 2011 lakini hajapata donge la kumfikisha nambari moja. Mauzo ya headphones zake za Beats by Dre kwa kampuni ya Apple yalimwezesha kuwa mwanamuziki wa kwanza aliyepata malipo ya juu zaidi kwa mwaka mmoja.

Anatarajiwa kuopokea zaidi ya dola milioni 100 kutoka kwa Apple. Itabainika wakati wa malipo hayo ikiwa atawapiku Diddy na Jay Z na kuingia nafasi ya kwanza.

Drake: Dola milioni 100 

Drake

Rapa huyo raia wa Canada alikuwa wa hivi punde kuingia kwenye orodha ya wanamuziki watano matajiri zaidi duniani mwaka uliopita. Muziki wake ndio unasikilizwa na kutazamwa zaidi duniani.

Rapa huyo anatajwa kuwa aliyejipa dola milioni 250 baada ya ushuru kutoka kwa bishara yake wa mvinyo na nyumba.

Eminem: Dola milioni 100 

Eminem

Licha ya kutofahamika saana kibiashara mwanamuziki huyo ameuza albamu nyingi zaidi kuliko rapa yeyote aliye hai na mwaka 2000 aliuza albamu nyingi ziadi kuliko mwanamuziki yeyote lakini hilo halikumpa nafasi katika orodha.

Kuingia katika orodha hii kunaripotiwa kutokana na mauzo ya albamu yake mpya – Revival