Wafahamu wanawake matajiri zaidi duniani na jinsi walipata utajiri wao

MacKenzie Bezos

Wakati mtu tajiri zaidi dunaini na mke wake waliamua kutalikiana bila shaka gharama ilitarajiwa kuwa kubwa.

Na hii ilithitishwa wiki hii wakati mwanzilishi wa kampuni ya Amazon Jeff Bezos na mke wake MacKenzie walikubaliana talaka.

MacKenzie Bezos atahifadhi asilimia 4 ya hisa zake katika kampuni ya Amazon, za thamani ya dola bilioni 35.6 na kumfanya kuwa mwanamke nambari tatu tajiri zaidi duniani na 24 kati ya watu matajiri duniani.

Lakini wanawake matajiri zaidi dunia ni kina nani na walipataje utajiri wao.

1) Françoise Bettencourt-Meyers

Utajiri: Dola bilioni 49.3 (pia yeye ni mtu nambari 15 tajiri duniani)

Yeye ni nani?

Mfaransa huyu alirithi kampuni ya bidhaa za urembo ya L’Oréal cosmetics akiwa yeye na familia yake wanamiliki asilimia 33 ya kampuni hiyo.

Mwanamke huyo mmwye maia 65 alirithi utajiri huo kutoka kwa mama yake Liliane Bettencourt,  ambaye alifariki Septemba 2017 akiwa na umri wa maiaka 94.

Wawili hawa hawakuwa na uhusiano mzuri tangu walipoanza kuzozana mwaka 2007, licha ya kupatana baadaye kabla ya kifo cha mama yake.

2) Alice Walton

Utajiri: Dola bilioni 44.4 (pia yeye ni mtu nambari 17 tajiri duniani)

Yeye ni nani?

Mwanamke huyu mwenye miaka 29 ni binti pekee wa Sam Walaton, mwanzilishi  wa maduka ya jumla ya Walmart.

Hata hivyo kinyume na ndugu zake wawili, amejitenga na kampuni hiyo ya kifamilia na kuangazia sana masuala ya sanaa akiwa sasa ni mwenyekiti wa kampuni ya Crystal Bridges ya sanaa za Marekani huko Bentonville, Arkansas.

3) MacKenzie Bezos

Utajiri: Takriban dola bilioni 35.6 ikiwa ni thamani ya hisa zake katika kampuni ya Amazon pekee lakini utajiri wake kamili unaweza kuwa wa juu.

Yeye ni nani?

Mwanamke huyu mwnye miaka 48 amezaa watoto wanne na mwanzilishi wa Amazon, ambaye walifunga ndoa mwaka 1993 baada ya kukuta wakifanya kazi pamoja katika kampuni tofauti.

Alikuwa mmoja wa wafanyakazi wa kwanza wa Amazon. Pia amechapisha vitabu viwili.

4) Jacqueline Mars

Utajiri: Dola bilioni 23.9 (pia yeye ni mtu nambari 33 tajiri duniani)

Yeye ni nani?

Mwanamke huyo mwenye miaka 79 anamiliki thuluthi moja ya kampuni kubwa zaidi ya kuoka mikate duniani iliyoanzishwa na na babu yake mwaka 1911.

Alifanya kazi na kampuni hiyo ya familia kwa karibu mika 20 na kubaki kwenye bodi hadi mwaka 2016.

5) Yan Huiyan

Utajiri: Dola bilioni 22.1 ambao umechangia awe mwanamke tajiri zaidi nchini China na mtu nambari 42 tajiri duniani.

Who is she? Yeye ni nani?

Mwanamke huyo mwenye miaka 37 ana hisa nyingi katika kampuni ya ujenzi ya kichina ya Country Garden Holdings.

Kulingana na na wavuti wake, Country Garden ilikuwa kampuni nambari tatu ya ujenzi duniani mwaka 2016.

Yan Huiyan, ambaye alifuzu kutoka Ohio State University, alirithi asilimia 57 ya kampuni hiyo kutoka kwa baba yake.

6) Susanne Klatten

Utajiri: Dola bilioni 21, utajiri unaomweka nambari 46 duniani.

Yeye ni nani?

Mwanamke huyu Mjerumani mwenye miaka 56 alirithi asilimia 50  katika kampuni ya kemikali ya Altana AG wakati wazazi wake walifariki. Pia yeye na ndugu wanamiliki asilimia 50 ya kampuni ya BMW.

7) Laurene Powell Jobs

Utajiri: Dola bilioni 18.6, kumfanya kuwa mtu nambari 54 tajiri duniani.

Yeye ni nani?

Mjane huyu wa mwanzilishi wa kampuni ya Apple, Steve Jobs, yeye na fammilia yake walirithi dola bilioni 20 katika kampuni ya Apple na Disney wakati mume wake alifariki.

Tangu wakati huo mwanamke huyu mwenye miaka 55 ameweka sehemu ya pesa katika uandishi wa habari.

Mei mwaka 2018 Powell Jobs alitumia dola milioni 16.8 kunua nyumba huko San Francisco.