Waarabu waapa kumng’oa Netanyahu mamlakani

Nipashe Online: Wabunge Waarabu nchini Israeli wamependekeza kuwa mkuu wa majeshi wa zamani Israeli Benny Gantz ndiye anayepaswa kuwa waziri mkuu wa Israeli.

Katika uchaguzi uliopita kiongozi wa Israeli Benjamin Netanyahu alikuwa bega kwa bega na Bwana Gantz, na wawili hao sasa wanawania kuunda serikali ya mseto.

Miongoni mwa vyama vilivyo katika orodha ya vile vitakavyounda serikali ya mseto ni pamoja na Muungano wa vyama vya waarabu ambavyo vilipata nafasi ya tatu vinavyosema vinataka kumuondoa mamlakani.

Hii ni mara ya kwanza tangu mwaka 1992 kwa kikundi cha wanasiasa wa kiarabu nchini Israeli kumuidhinisha waziri mkuu

Huu ulikuwa ni uchaguzi mkuu wa pili wa mwaka wa Israeli . Baada ya uchaguzi wa kwanza , mwezi April , mazungumzo ya muungano yalivunjika kna uchaguzi ukaitishwa.

Reuven Rivlin with members of the Joint List alliance at a long tableHaki miliki ya pichaEPA-Muungano wa vyama mseto ukiwasilisha mapendekezo yao kwa Reuven Rivlin

Akikabiliwa na mkwamo mwingine wa kisiasa , rais Israel Reuven Rivlin amependekeza kuwepo kwa serikali mpya itakayojumuisha miungano yote ule wa Blue wa Gantz na ule wa White pamoja na chama cha wazri mkuu Bwana Netanyahu cha Likud.

Bwana Rivlin amekwishasema kuwa atafanya kila liwezekanalo kuepuka uchaguzi mkuu wa tatu nchini Israeli mwaka huu .

Aymen Odeh, kiongozi wa mungano , amemuambia Rivlin kwamba kipaumbele cha muungano wao ni kumzuwia Bwana Netanyahu kuongoza kwa muhula mwingine.

Muungano huo wa vyama vya kiarabu una viti 13 bungeni . Bwana Gantz aliidhinishwa na wabunge wote 13 , lakini bado atahitaji viti 61 vinavyohitajika kupata wingi wa viti katika bunge la Israeli lenye viti 120.

Huu ni mchakato muhimu wa mamlaka ya kisiasa kwa raia wa Palestina ndani ya Israel

Rais Rivlin anashauriana na viongozi wa chama kuhusu ni nani ambaye atamuomba kuongoza nchi baada ya matokeo ya uchaguzi wa wiki iliyopita ambao hayakutoa matokeo kamili . Vyaka vya kiarabu vimeonyesha nguvu kwa kuwa namba tatu kwa idadi ya viti vya bunge.

Benjamin Netanyahu na Benny GantzHaki miliki ya picha REUTERS-Benjamin Netanyahu na Benny Gantz

Uungaji mkono wao hautampa wingi wa viti Benny Gantz na muungano wa Blue & White , lakini utamuinua katika mazungumzo kuhusu ni nani atapata nafasi ya kwanza ya kuunda serikali.

Kiongozi anayehusika na uundaji wa makundi ya waarabu nchini Israeli , Ayman Odeh, anasema hawamuidhinishi Bwana Gantz na sera zake, lakini wanafanya juhudi za kujaribu kumzuwia Benjamin Netanyahu kupata muhula mwingine madarakani, na vilevile kutuma ujumbe wa wazi kwamba hali ya baadae ya Israeli lazima ijumuishe ushirikishwaji sawa na kamili wa raia wake wa kipalestina.

Akizungumza na wafuasi wakati wa kampeni za uchaguzi , Netanyahu alisema: “Sote tumepitia kampeni ngumu ya uchaguzi.

“Bado tunasubiri matokeo yenyewe, lakini jambo moja li wazi. Hali nchini Israel ipo katika kiwango cha historia, tumekabiliwa na changamoto nyingi na fursa nyingi.”

Kwa upande wake bwana Gantz alionekana kuwa na matumaini zaidi alipozungumza na wafuasi wake mapema kidogo.

“Bila shaka tutayasubiri matokeo halisi, lakini inavyoonekana ni kana kwamba tumelifikia lengo letu,” amesema.

“Umoja na utangamano upo mbele yetu.”