Virusi vya Zika kutibu saratani ya ubongo

Kirusi hatari ambacho kinaweza kusababisha madhara makubwa kwa watoto cha Zika, kinaweza kusaidia kutibu saratani ya ubongo miongoni mwa watu wazima, kwa mujibu wa wanasayansi wa Marekani.

Hadi sasa Zika imekuwa tisho kubwa kwa dunia.Lakini utafiti mpya unaonyesha kuwa kirusi hicho kinaweza kukula na kuua seli hatari za saratani ya ubongo kwa watu wazima.

Ingawa bado binadamu hajafanyiwa utafiti huo, wataalamu wanaamini kwa virusi vya Zika vinaweza kuwekwa kwa ubongo na kuua seli hatari za saratani ya ubongo.

Kuna aina tofauti za saratani ya ubongo zinazomuathiri mwanadamu. Ugonjwa aina ya Glioblastomas ndio huaathiri zaidi watu wazima na mgumu zaidi kutibiwa.

Seli zake hukua kwa haraka kwenye ubongo ikimaanisha kuwa ni vigumu kubaini seli hizo zimemea wapi au kuishia wapi.

Mbinu za kitubu saratani hiyo zikiwemeo za Radiotherapy, chemotherapy na upasuaji  haziwezi kusaidia kuondoa kabisa seli za saratani.

Lakini utafiti wa hivi punde unaonyesha kuwa virusi vya Zika vinazaweza kuua seli sugu za saratani ya ubongo.