Virgil van Dijk kuwafunika Tena Messi, Ronaldo tuzo za FIFA?

Nipashe Online: Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani FIFA limetangaza majina matatu yakayaoingia kwenye kinyang’anyiro cha kuwania uchezaji bora wa shirikisho hilo katika ngazi ya klabu na timu ya taifa.

Mlinzi wa Liverpool na timu ya taifa ya Uholanzi Virgil van Dijk ametajwa kwenye orodha ya
wachezaji watatu sambamba na mchezaji bora mara tano ulaya Lionel Messi (Barcelona na
Argentina) na Cristiano Ronaldo (Juventus na Ureno).

Katika tuzo hizo pia mlinzi wa timu ya taifa ya England ya Wanawake Lucy Bronze ametajwa kuwania tuzo sawa na kocha wake Phil Neville aliyeifikisha timu hiyo nusu fainali ya kombe la dunia.

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola, kocha wa Liverpool Jurgen Klopp na Bosi wa Tottenham Mauricio Pochettino wameingia katika orodha ya mwisho ya makocha bora upande wa wanaume.

Washindi watatangazwa jijini Milan Italia mnamo Septemba 23 mwaka huu.

TUZO ZA FIFA KWA UJUMLA WAKE

TUZO ZA WACHEZAJI WA KIUME:-

Cristiano Ronaldo (Juventus/Ureno), Lionel Messi (Barcelona/Argentina), na Virgil van Dijk
(Liverpool/Uholanzi)

KOCHA BORA:

Pep Guardiola (Manchester City), Jurgen Klopp (Liverpool), na Mauricio Pochettino (Tottenham)

KIPA BORA:

Alisson (Liverpool/Brazil), Ederson (Manchester City/Brazil), na Marc-Andre ter Stegen
(Barcelona/Germany)

TUZO KWA WANAWAKE:

Lucy Bronze (Lyon/England), Alex Morgan (Orlando Pride/USA), na Megan Rapinoe (Reign FC/USA)

KOCHA WA BORA UPANDE WA TIMU ZA WANAWAKE:

Jill Ellis (USA), Phil Neville (England), Sarina Wiegman (Uholanzi)

Mlinda Mlango Bora Kwa Wanawake:

Christiane Endler (Paris St-Germain/Chile), Hedvig Lindahl (Wolfsburg/Sweden), na Sari van Veenendaal (Atletico Madrid/Uholanzi)

GORI BORA LA MSIMU(PUSKAS AWARD):

Lionel Messi (Barcelona v Real Betis), Juan Quintero (River Plate v Racing Club), na Daniel Zsori (Debrecen v Ferencvaros)

Mwandishi: Bruce Amani