Vikosi vya usalama vyaua zaidi ya watu 100 katika maandamano Iraq

Nipashe Online: Maandamano dhdi ya serikali nchini Iraq yaliingia siku ya tano jana Jumamosi katika mji mkuu Baghdad na majimbo mengine huku waandamanaji wakichoma moto ofisi za umma na kupuuza miito ya utulivu kutoka viongozi wa kisiasa na dini.

Maafisa wa usalama waliwaua kwa risasi waandamanaji 19 na kujeruhi wengine zaidi ya 30 katika machafuko ambayo watu 100 wamekufa na wengine 4000 kujeruhiwa, tangu yalipozuka siku ya Jumanne, kupinga vitendo vya rushwa, ukosefu wa ajira na huduma duni za kijamii.

Hapo jana viongozi wa kisiasa walishindwa kuitisha kikao cha dharura cha bunge kujadili matakwa ya waandamanji, baada ya kiongozi wa walio wengi bungeni Muqtada al-Sadr kuamuru kikao hicho kisusiwe.

Siku ya Ijumaa Al-Sadr alitoa wito wa kujiuzulu kwa serikali ya waziri mkuu Abdul-Mahdi na kuitishwa uchaguzi wa mapema akisema umwagaji damu wa raia haupaswi kupuuzwa.