Ugonjwa wa Malaria kutokomezwa ifikapo 2050

Nipase Online: Wataalamu wa afya duniani wanasema Malaria inaweza kutokomezwa katika kizazi kijacho. Kwenye ripoti iliyochapishwa jana Jumapili, wataalamu 41 wamesema ugonjwa wa malaria hautokuwepo ifikapo mwaka 2050.

Ripoti hiyo iliyochapishwa na jarida la matibabu la Lancet, imesema ili kulifika lengo hilo, serikali, wataalamu na wahudumu wa afya wanahitaji kuwekeza zaidi kifedha a kiuvumbuzi katika kupambana na ugonjwa huo unaoambukizwa na mbu.

Malaria imewaathiri watu wapatao milioni 219 mwaka 2017, na kusababisha vifo vya watu 435,000 wengi wao wakiwa ni watoto wadogo na watoto wachanga katika mataifa maskini barani Afrika.