Ugongwa wa kipindupindu wazuka Musumbiji baada ya kimbunga

Mamlaka nchini Musumbiji zinasena kuwa ugonjwa wa kipindupindu umezuka baada ya nchi hiyo kukumbwa na kimbunga Idai.

“Tuna visa vitano vya kipindupindu ambavyo vimethibitishwa. Hii ni pamoja na katika mji wa Beira na maneo yanayuozunguna,” waziri wa mazingira Celso Correia alinukuliwa na AFP.

Zaidi ya watu 450 nchini Musumbiji walifariki kutokana na kimbunga hicho ambacho kiliharibu nyumba na kusababisha mafuriko sehemu za Beira na maeneo mengi yaliyo karibu.