Uber kuacha kutumia magari ya diesel London 2019

Kampuni ya teksi ya Uber, itaacha kutumia magari ya diesel mjini London ifikapo mwishoni mwa mwaka 2019, na magari mengi yatakuwa ni yale yanayotumia umeme au umeme na mafuta.

Kwa sasa kampuni hiyo inasema kuwa karibu nusu ya safari zote zilizofanywa mjini London hufanywa na magari yasiyotumia mafuta na yenye huduma nafuu ya Uber, ambayo huwawezesha wateja kuagiza teksi kupitia kwa simu zao.

Makampuni mengi ya kuunda magari yatangaza mipango miezi ya hivi karibuni ya kuunda magari mapya yanayotumia umeme huku kampuni ya Volvo ikiwa ndiyo ya kwanza kubwa kutangaza tarahe ya kuacha kuunda magari yanayotumia mafuta.

Uingereza itapiga marufuku mauzo ya magari mapya yanayotumia mafuta kuanzia mwaka 2040 na kufuata hatua za Ufaransa, na miji kama ,Madrid, Mexico City na Athens.

 Uber ambayo ina madereva 40,000 mjini London, itatoa huduma kwa kutumia magari yasiyotumia mafuta kwa muongo mmoja unaokuja na ina mipango ya kufanya hivyo ifikapo mwaka 2022 kote nchini.