Trump athibitisha kuwa mwanawe Osama Bin Laden aliuawa

Hamza Bin Laden

Nipashe Online: Rais awa Marekani Donald Trump amethibitisha kwamba Hamza Bin Laden mwana wa mwanzilishi wa kundi la Al Qaeda Osama Bin Laden aliuawa katika operesheni ya Marekani.

Mwezi uliopita vyombo vya habari vya Marekani vilinukuu duru za kijasusi ambazo ziliripoti kwamba aliuawa katika shambulio la angani.

Alitajwa na Marekani kuwa gaidi miaka miwili iliopita. Alionekana kuwa mrithi wa moja wa moja wa babake.

Akidaiwa kuwa na umri wa miaka 30 alikuwa ametoa wito wa mashambulizi dhidi ya Marekani na mataifa mengine.

”Hamza Bin Laden kiongozi mkuu wa al-Qaeda na mwana wa Osama bin Laden aliuawa katika shambulio la operesheni ya Marekani dhidi ya ugaidi nchini Afghanistan / Pakistan”.

Bwana Trump alizungumza katika taarifa fupi iliotolewa na Ikulu ya Whitehouse.

Kifo cha Hamza kinainyima Al – Qaeda uongozi muhimu na uhusiano wa babake lakini pia kinakandamiza operesheni na vitendo vya kihalifu vya kundi hilo.

Taarifa hiyo haikutoa mda wa operesheni hiyo. Mwezi Februari Marekani ilikuwa imetoa ofa ya $1m kwa habari ambayo ingepelekea kukamatwa kwa Hamza

Hamza Bin Laden alionekana kuwa kiongozi chipuka wa al- Qaeda .

Osama Bin Laden

Iliripotiwa mwezi Agosti kwamba alikuwa ameuawa na operesheni ya kijeshi katika kipindi cha miaka miwili iliopita na serikali ya Marekani ilihusika lakini muda na tarehe haikujulikana.

Wasifu wa Osama bin Laden

Bin Laden aliwahi kunukuliwa akisema: “Kile ambacho Marekani inakionja hivi leo ni kitu kidogo sana ikilinganishwa na kile ambacho tumekuwa tukikipata katika miongo kadhaa. Taifa letu limekabiliwa na hali hii ya kudhalilishwa na kudharaualiwa kwa zaidi ya miaka 80. Wanawe wanauwawa, damu yao inamwagwa, maeneo yake matakatifu yanahujumiwa na hayatawaliwi kwa mujibu wa amri zake Mwenyezi Mungu.”

Osama bin Laden alizaliwa mwaka 1957 katika familia yenye utajiri mkubwa. Baba yake alianzisha kampuni kubwa ya ujenzi katika Saudi Arabia. Akiwa ni miongoni mwa ndugu 18 wa kiume, Osama aliwahi kufanya kazi katika biashara hiyo ya familia. Maisha yake yalianza kubadilika alipokuwa kijana pale Muungano wa Sovieti ulipoivamia Afghanistan.

Alipokwenda Aghanistan, Osama alikuwa kijana sana ambaye alitaka kujijengea umaarufu, katikati ya vita vitakatifu. Osama bin Laden alikaa kwa kipindi cha takriban miaka 10 nchini Afghanistan, na kuanzisha fungamano na wanaharakati wa siasa kali za kiislamu kote duniani.

Na baada ya majeshi yaliyovunjika moyo ya Sovieti kuondoka Afghanistan mnamo mwaka 1989. Osama bin Laden alirejea nyumbani Saudi Arabia. Mwaka mmoja baadaye alijitolea kumpa msaada wa kijeshi mfalme Fahad wakati Iraq ilipoivamia nchi jirani ya Kuwait. Lakini Osama alipatwa na mshtuko mkubwa pale Mfalme Fahad alipokataa toleo lake na badala yake kuigeukia Marekani.

Osama alinyaganywa uraia wa Saudi na akarejea Afghanistan ambayo wakati huo ikitawaliwa na Wataliban ambao alikubaliana nao kuhusu tafsiri ya uislamu.

Mnamo mwaka 1998 aliwahimiza waislamu wawauwe Wamarekani mkiwemo raia popote pale watakapowapata, kukafuatiwa mashambulio kadhaa ikiwa ni pamoja na dhidi ya balozi za Marekani katika Kenya na Tanzania na manowari ya USS Cole katika mwambao wa Yemen. Halafu shambulio la September 11, 2001.

Nyumba ya ghorofa ambamo bin Laden anaaminika alikutwa na kuuawa.Haki miliki ya picha OTHER

Osama bin Laden aliwasifu waliofanya shambulio hilo. Rais Bush akasema atasakwa apatikane akiwa hai au mfu.

Rais Bush alikunukuliwa kusema: “Sijui kama tutampata kesho au mwezi ujao au mwaka ujao. Lakini hapana shaka tutampata tu.”

Ingawa Waislamu wengi walilaani vifo vya watu katika miji ya New York na Washington, Osama bin Laden alichukuliwa na wengi kuwa ni shujaa, aliyetetea haki za Wapalestina na kupinga nguvu za Marekani.

Alioa mke wake wa kwanza akiwa na umri wa miaka 17 na baadaye akawaoa wake wengine wanne. Osama bin Laden anaaminika kuacha watoto 17.