Trump anasema hataki vita na Iran baada ya mashambulizi Saudi Arabia

Nipase Online: Rais wa Marekani Donald Trump amesema kwamba hataki vita na Iran. Hii ni baada ya mashambulizi katika visima viwili vya kuzalisha mafuta huko Saudi Arabia.

Akizungumza katika ikulu ya White House Trump amesema kuwa atajaribu kuepuka vita vya aina hiyo.

Kulingana na Trump uchunguzi bado unaendelea kubaini hasa nani aliyehusika na mashambulizi hayo ya Jumamosi huko Saudi Arabia.

Waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran nchini Yemen walikiri kuhusika na shambulizi hilo.

Lakini Waziri wa Mambo ya nje wa Saudi Arabia amesema kwamba silaha za Iran ndizo zilizotumika katika kufanya mashambulizi hayo.