Trump aamuru vikwazo vikali zaidi dhidi ya Iran

Nipashe Online: Rais Donald Trump wa Marekani ametangaza vikwazo vipya dhidi ya Iran kufuatia mashambulio katika visima vya mafuta vya Saudi Arabia.

Rais Trump amesema amemtaka waziri wake wa Fedha Steven Mnuchin ahakikishe vikwazo hivyo vinakuwa vikali zaidi. Vielelezo vya vikwazo hivyo bado havijulikani.

Rais huyo wa Marekani amesema uwezekano wa kujibu shambulizi hilo kijeshi ni njia ya mwisho.

Bado pande hizo mbili zinazohasimiana zinaendelea kubishana kuhusu nani walikuwa nyuma ya mashambulio dhidi ya vinu vya mafuta vya Saudi Arabia.

Waasi wa Houthi nchini Yemen wanadai walihusika na mashambulio hayo . Marekani lakini inailaumu Iran kuwa nyuma ya mashambulio hayo.