Tamasha lijalo la Nicki Minaj Saudi Arabia lazua gumzo mitandaoni

Nipashe Online: Tangazo la kuwa Nicki Minaj atakuwa mmoja ya wasanii watakaotumbuiza katika tamasha la muziki nchini Saudi Arabia, limezua gumza kali katika mitamdao ya kijamii nchini humo.

Mtindo wake wa mavazi na maudhui ya ngono katika nyimbo zake ni baadhi ya masuala watu wana hoji huku wakitafakari tamasha hilo litapokelewaje katika jamii hiyo ya khafidhina.

Rapa huyo anatarajiwa kutumbuiza watu katika tamasha la Jeddah World Fest Julai 18.

Tamasha hilo ni mfano wa hivi karibuni wa jinsi Saudi Arabia inavyoendelea kulegeza msmamo wake mikali hasa katika masuala ya burudani ili kuimarisha ukuaji wa sekta ya sanaa.

“Nicki Minaj” alitrend katika mtandao wa Twitter baada tamasha lake la Jeddah kutangazwa.

“Hebu tafakari kupata fahamu baada ya kupoteza fahamu kwa miaka mitatu na ukizinduka kitu cha kwanza unasikia ni kuwa Nicki Minaj atafungua tamasha la muziki Saudi Arabia, kusema kweli nitafikiria niko katika taifa lingine ,” mmoja aliandika.

Mwingine alihoji ikiwa waandalizi wa tamasha hilo walifanya ukaguzi wa maonesho yake yaliopita japo angalau katika mtandao wa Google kabla ya kumpa kazi hiyo. “Hivi hakuna mtu Saudi Arabia aliyemtafuta Nicki Minaj kwenye google?” aliandika Kabir Taneja.

Sio maoni yote yalikuwa ya kufanya mzaha. Mtu mmoja aliandika katika Twitter yake kuwa tamasha hilo la Minaj halitakuwa sawa hasa ikizingatiwa kuwa litafanyika karibu na mji Mecca- amabo ni mtakatifu kwa waumini wa Kiislam .

Katika video iliyowekwa kwenye Twitter mwanamke aliyevalia mavazi ya kidini alihoji kwa nini mamlaka ya nchini humo inamrusu rapa huyo kutumbuiza katika tamasha hilo huku ukiwazuia wanawake kuvaa mavazi yanayowabana hadharani.

“Atakuja kutingiza makalio yake na akiimba nyimbo zake zilizo na maudhui ya ngono huku akijitingisha zaidi,” alisema “Halafu unaniambia mimi nivae abaya. Hilo linaingia akini kweli ?”

Wengine walisema hatua ya mwanamuziki huyo kufanya tamasha nchini humo ni unafiki, ikizingatiwa kuwa anatumbuiza piakatika matamasha ya wapenzi wa jinsia moja ili hali anajua msimamo wa Saudia kuhusu uhusiano wa aina hiyo. Hukumu ya kushiriki mapenzi ya jinsia moja nchini Saudia Arabia ni kifo.

Mariah Carey alipuuza wito wa wanaharakati wa kutetea haki za binadamu kumuomba afutilie mabali tamasha lake nchini Saudia huku rapa Nelly nae akilaumiwa vikali kwa kuandaa tamasha la wnaume pekee.

Hatua ya hivi karibuni ya kulegeza misimamo kuhusu masuala tofauti ya kijamii ikiwemo burudani ni sehemu ya mkakati wa mwanamfalme Mohammed bin Salman wa kuimarisha uchumi wa nchi hiyo.

Turki Al al-Sheikh, mkuu wa kitengo cha burudani alitangaza kuhusu mpango wa siku zijazo wa kufanyia mageuzi sekta ya muziki katika ujumbe wa Twitter mwezi Januari.

“Mungu akijaalia, hatua itakayofuatia katika masuala ya burudani siku zijazo ni maonesho kutoka kwa watumbuizaji tofauti, michezo ya watoto katika maeneo yalio na bustani pamoja na michezo mingine mingi itakyowasaidia vijana, wanawake na wanaume kusaidia kampuni za kitaifa za burudani,” aliandika.

Umoja wa Mataifa pamoja na mashirika mengine ya kutoa misaada ya kibinadamu yameonya kuwa mikasa kama hii haiwezi kuepukika mapigano yakizuka upya katika mji wa Tripoli ambako wahamiaji wanazuiliwa katika vituo vilivyo karibu na maeno mapigano yanaendelea.

Hali ya wahamiaji kutokea mwanzoni ilikuwa mbaya na badhi yao wamekuwa wakidhulumiwa na watekaji nyara na wanamgambo.

Umoja wa Mataifa unasema mashambulio ya anagani dhidi ya Tajoura yanaonesha kuwa sera ya Umoja wa Ulaya ya kuwaregesha Libya watu wanaojaribu kuvuka bahari Mediterrania kuingia Ulaya lazima ikomeshwe .

Sera hiyo imesaida kupunguza idadi ya watu wanaoingia barani ulaya kupitia njia hiyo japo zingine zimefunguliwa.

Lakini mshirika ya kutoa misaada ya kiutu yansema gharama ya kutekeleza sera hiyo ni ghali mno.

Baada ya oparesheni ya Jenerali Khalifa Haftar katika mji wa Tripoli kutibuka, kuna uwezekano wa vikosi vyake kushambulia watu kiholela hali ambayo itahatarisha zaidi maisha ya raia.

Lakini wanamgambio wanaowazuilia wahamiaji katika mazingira hatari karibu na eneo la vita, sharti walaumiwe chochote kikitokea