Saudi Arabia yasema kuna uwezekano wa kuishambulia Iran

Nipashe Online: Waziri wa maswala ya kigeni nchini Saudia amesema kwamba watatumia mbinu yoyote kujibu mashambulizi ya hifadhi zake za mafuta , ikiwemo jibu la kijeshi baada ya kuilaumu Iran kwa kutekeleza shambulio hilo.

Huku Saudia ikitaka kuzuia kutokea kwa vita, Iran itawajibishwa kwa shambulio la ndege isio na rubani inayobeba silaha na mashambulio ya makombora katika hifadhi zake za mafuta kulingana na Adel al-Jabeir aliyezungumza na BBC.

Uchunguzi wa Marekani uliodai kwamba Iran ilihusika uliungwa mkono na Uingereza, Ufaransa na Ujerumani wiki hii.

Iran imekana kuhusika na shambulio hilo.

Waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran ambao wanakabiliana na muungano wa majeshi yanayoongozwa na Saudia wamesema kwamba walitekeleza shambulio hilo katika visima hivyo vya mafuta.

Lakini maafisa wa Saudia wanasema kwamba kiwango, na uharibu wa shambulio hilo unashinda uwezo wa waasi wa Houthi.

Saudia imesema kuwa kuna uwezekano wa shambulio la kijeshi dhidi ya Iran

Akizungumza na mwandishi wa BBC anayehusika na maswala ya kimataifa Lyse Doucet katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York , bwana Jubeir alisema: Kila mtu anajaribu kukwepa vita na kusambaa kwake.

Hivyo basi tutazama mbinu zote zilizopo kwetu. Tufanya uamuzi wakati unaofaa. Aliongezea: Kuomba radhi kwa Iran hakujafanikiwa katika siku za nyuma na hakutaisadia katika siku za usoni.

Marekani iliiongezea vikwazo vya kiuchumi Iran mwaka uliopita baada ya kujiondo katika makubliano ya kinyuklia ya mwaka 2015 na mwezi Mei ilisema italazimisha matiafa yote kukoma kununua mafuta ya Iran ili kuishinikiza kurudi katika meza ya majadiliano ya mkataba mpya wa kinyuklia.

Siku ya Jumatano , waziri wa maswala ya nchi za kigeni Mike Pompeo aliambia wanahabari katika umoja wa mataifa UN kwamba Marekani ilitaka mwafaka wa amani na taifa la Iran.

”Mwishowe itakuwa ni Iran yenye kufanya maamuzi , iwapo watachagua ghasia na chuki”, aliongezea.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alijaribu kufanya mkutano kati ya rais wa Iran Hassan Rouani na mwenzake wa Marekani Donald Trump.

Hassan Rouhani akizungumza katika makao makuu ya Umoja wa mataifaHaki miliki ya picha EPA – Rais wa Iran amekataa kukutana na rais Trump

Lakini bwana Rouhani aliambia wajumbe katika Umoja wa mataifa kwamba alikataa kukutana na bwana Trump kutokana na vikwazo vya taifa hilo vinavyoendelea kulikabili taifa hilo.

Kwa kuwa vikwazo vya uchumi vilivyowekwa dhidi ya taifa hilo vinaendelea.

Alitoa shaka juu ya nia ya Marekani, akimaanisha kujivuna kwa Bwana Pompeo siku ya Jumatano kwamba ilikuwa “imeweka vikwazo vikali katika historia” kwa Irani.

“Mtu anawezaje kuwaamini wakati wa ukandamizaji wa kimya wa taifa kubwa, na shinikizo kwa maisha ya watu milioni 83 wa Iran, haswa wanawake na watoto, unaungwa mkono na maafisa wa serikali ya Marekani?” alisema. “Taifa la Iran halitawahi, kusahau na kusamehe uhalifu huu na wahalifu hawa.”

Pia alifutilia mbali wazo la kupiga picha na Rais Trump, ambaye amechukua fursa kadhaa za kupiga picha na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un – ikiwemo moja iliopigwa katika eneo linalolindwa sana la mpakani katika rasi Korea (DMZ).

“Picha kama hizo zinafaa kupigwa baada ya kumalizika kwa majadiliano , sio kabla ya majadiliano,,” Bwana Rouhani alisema.