Jeshi la Algeria sasa linataka Rais Abdel Aziz Bouteflika kuondolewa ofisini

Rais wa Algeria Abdel Aziz Bouteflika

Mkuu wa majeshi nchini Algeria ametaka kutumiwa katiba ambapo Rais Abdel Aziz Bouteflika atatangazwa asiyestahili kuendelea kuwa ofisini katika hatua ambayo ni nadra sana kuchukuliwa na jeshi baada ya wiki kadhaa za maandamano.

Maelfu ya watu wamekuwa wakiandamani wakitaka utawala wa miaka 20 wa rais huyo mwenye miaka 82 na kundi lote ambalo limekuwa ofisini tangu nchi ipate uhuru kutoka Ufaransa mwaka 1962.

Licha ya jeshi kuwasifu waandamanaji, lilionya kuwa ghasia haziwezi kuvumiliwa

Akiwahutubia maafisa wa jeshiLuteni Jerenali  Ahmed Gaed Salah, alitoa wito wa kuwepo hatua ya pamoja kutatua mzozo unaokumba taifa hilo la kaskazini mwa Afrika ambayo ni mzalishaji wa mafuta na gesi.

Kulingana na kipengee cha 102 mwenyekiti wa bunge la juu Abdelkader Bensalah, atahudumu kama rais kwa takriban siku 45 wa taifa hilo lenye karibu watu 40.

Runinga ya El Bilad ilisema baraza la katiba lilikuwa limefanya kikao maalum baada ya mkuu wa majeshi kuingilia kati.