Samaki wanaogeukia pombe ili kuishi

Wanasayansi wamebaini siri ya samaki wa dhahabu jinsi wanavyoweza kuishi chini ya maziwa yaliyofunikwa na barafu.

Watafiti hao pia wamebaini kwa nini samaki na ni jinsi gani samaki hao hugeuza asidi ya lactic kwenye miili yao kuwa pombe, kama ya njia ya kuwawezesha kuendelea kuwa hai.

Baadhi ya samaki hao waligunduliwa kuwa na viwango vya juu vya pombe kushinda kiwango dereva anachostahili kuwa nacho kwenye damu anapoendesha gari katika nchi nyingi.

Watafiti hao wamesema utafiti huo unaweza kuwasaidia kufanya utafiti zaidi kuhusiana na madhara yanayotokana na pombe kwa binadamu.

Wanasayansi wamekuwa anafahamu kuhusu uwezo wa kipekee wa samaki hao wa dhahabu kuweza kuishi maeneo yenye hali ngumu ya kimazingira na wenzao wa baharini aina ya Crucian Carp tangu miaka ya 1980.

Ingawa binadamu na wanyama wengine wenye uti wa mgongo hufariki muda mfupi baada yao kukosa hewa ya okisejeni, samaki hawa wana uwezo wa kuishi katika mazingira hayo ya barafu kwa miezi kadhaa katika bahari kaskazini mwa bara Ulaya.

Watafiti hao wamebaini jinsi wanyama hao hutumia mbinu maalum kuwawezesha kuendelea kuishi katika mazingira hayo.

Kwa wanyama wengi kuna aina moja ya protini ambayo hutumiwa kuelekeza wanga (kabohaidreti) kwenye mitochondria, viungo vinavyotumiwa kuzalisha kawi kwenye seli.

Iwapo hakuna hewa ya okisejeni, kutumiwa kwa wanga kuzalisha nishati huzalisha asilidi aina ya alctic ambayo samaki hawa huwa hawawezi kuiondoa mwilini.

Asidi hiyo huua kiumbe baada ya dakika chache.

Kwa bahati nzuri, samaki hao wa dhahabu wamebadilika na kuwa na seti ya pili ya protini ambayo inaweza kufanya kazi hata okisjeni ikiwa haipo na huibadilisha asidi ya lactic kuwa pombe, ambayo baadaye hutolewa mwilini kupitia kwenye yavu yavu za samaki hao.