Reli mpya ya Kenya ilipata hasara ya dola milioni 100 mwaka wa kwanza

Mradi mpya wa reli nchini Kenya umepata hasara ya dola milioni 100 mwaka wake wa kwanza kwenye huduma, kwa mujibu wa wizara ya uchukuzi.

Mradi huo unaofadhiliwa na China unafahamika kama standard gauge railway – na unaunganisha miji ya Mombasa na Nairobi na ulifadhiliwa kwa kima cha dola bilioni 3, mkopo kutoka beki ya China ya Exim, unaotakiwa kulipwa ndani ya kipindi cha miaka 15.

 

Kenya ilikana madai kuwa mradi huo uligharimu pesa nyingi kupindukia, usiokuwa wa maana na usio na manufaa kiuchumi.

Reli hiyo ilikuwa kiungo muhimu cha kampeni ya Rais Uhuru Kenya uchaguzi mkuu uliopita na ilizinduliwa miezi michache kabla ya kufanyika kwa uchaguzi.

Licha ya treni za abiria kuwa na wateja wengi kila mara waziri alisema kuwa imekuwa vigumu kuwashawishi wafanyabiashara kusafiriusha mizigo yao kwa kutumia reli badala ya kutumia barabara.

Waziri wa uchukuzi James Machari aliiambia kamati ya  bunge kuwa serikali sasa iko kwenye mazungumzo na sekta za binafsi kuhusu namna ya kuweza kunufaika kutoka na na usafiri wa reli.

Malipo ya mkopo huo yananza mwaka ujao na kama reli yenyewe haitalipa mkopo huo basi walipa kodi watahitajika kuulipa.