Rais Magufuli: Wafungwa wafanye kazi ngumu na wazembe wapigwe mateke

Rais Magufuli

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amesema kuwa wafungwa wanapaswa kufanyishwa kazi usiku na mchana na kwamba wafungwa wazembe wanafaa ‘kupigwa mateke’.

Magufuli alikuwa akizungumza katika uzinduzi wa afisa mkuu mpya wa Magereza nchini humo .

Amesema kuwa ilikuwa aibu kwa Tanzania kuendelea kuwaachilia huru wafungwa na kwamba watu hao wanapaswa kulima chakula chao katika shamba.

Anasema kuwa kutofanyishwa kazi kwa wafungwa kumesababisha kuwepo kwa wapenzi wa jinsia moja na matumizi ya mihadarati katika jela.

Ametoa wito wa kusitishwa kwa wanawake au wanaume kutembelea wake zao au waume zao jela.

Makundi ya wanaharakti yamemshutumu kiongozi huyo kwa kushindwa kuwavumilia wapinzani wake wa kisiasa , makundi ya wapenzi wa jinsia moja na makundi mengine.