Pakistan yaonya juu ya kushambuliwa na India

Waziri mkuu wa Pakistan Imran Khan

Nipashe Online: Waziri mkuu wa Pakistan amesema ameionya Jumuiya ya Kimataifa kwamba India huenda ikaanzisha shambulio dhidi ya jimbo la Kashmir linaloshikiliwa na Pakistan kama juhudi za kuwaondowa watu katika kumulika vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu unaofanywa na nchi hiyo kwenye sehemu ya jimbo linalozozaniwa la Himaya ambalo linadhibitiwa na India.Pa

Katika hotuba yake Imran Khan mjini Islamabad amesema nchi yake itaijibu kwa njia stahiki serikali ya waziri mkuu Narendra Modi ikiwa itaishambulia Pakistan.

Kadhalika Waziri mkuu Khan amesema mgogoro wa aina yoyote kati ya nchi hizo mbili zinazomiliki silaha za Nyuklia hautokuwa na matokeo mazuri kwa eneo la ukanda wa Kusini mwa Asia lakini pia dunia kwa ujumla itaathirika.

Amebaini kwamba atalizungumzia suala hilo atakapohutubia mkutano wa hadhara kuu ya Umoja wa Mataifa mwezi Ujao.