Pakistan yafanya jaribio la makombora ya nyuklia

Nipashe Online: Msemaji wa jeshi la Pakistan Meja Jenerali Asif Ghafoor amesema jeshi limefanikiwa kufanya jaribio la hatua kwa hatua la kombora la nyuklia, wakati ambapo kunashuhudiwa mvutano kati yake na jirani yake India juu ya eneo linalo-zozaniwa la Kashmir.

Amesema jaribio la kombora hilo lililofanyika usiku lina uwezo wa kubeba silaha na kufikia umbali wa kilomita 290.

Zoezi hilo linakuja wakati uhasama kati ya Pakistan na India ukiongezeka kufuatia India kufuta hadhi ya kujitawala yenyewe jimbo la Kashmir.

Pakistan ilijibu kwa hasira uamuzi huo wa India, kwa kusitisha huduma za usafiri na mahusiano ya kibiashara kati ya mataifa hayo mawili pamoja na kumfukuza balozi wa India nchini Pakistan.