Ofisi ya Tume ya Uchaguzi nchini Nigeria yachomwa moto siku 6 kabla ya uchaguzi

Ofisi ya tume ya uchaguzi nchini Nigeria imechomwa moto siku sita kabla ya nchi hiyo kuandaa uchaguzi mkuu.

Moto katika jimbo la Plateau umeharibu kila kitu kilichohitajika kupiga yakiwemo masanduku na makaratasi ya kupigia kura.

Msemaji alitaja kisa hicho kuwa pigo kwa maandalizi kwa uchaguzi lakini amenukuliwa akisema ni mapena sana kushuku kuwa ilikuwa ni hujuma.

Uchaguzi mkuu unarajiwa kuandaliwa siku ya Jumamosi.

Siku ya Jumapili Rais Muhammadu Buhari alionya kuhusu uwezekano wa kuwepo udanganyifu wakati wa kura.

Anawania tena kwenye uchaguzi huo ambao watu milioni 84 wamesajiliwa kupiga kura.

Licha ya kuwepo wagombea wengi wa urais, wadadisi wanasema mshindani mkuu wa Bw Buhari ni makamu rais wa zamani Atiku Abubakar.