Nicki Minaj anasema atastaafu ili kuanza familia

Nipashe Online: Nicki Minaj anasema kwamba ameamua kustaafu ili kuanzisha familia yake na akawaambia mashabiki wake kwamba anawapenda ‘maisha yake yote’.

Mshindi huyo wa tuzo ya Grammy anachumbiana na mwanamume kwa jina Kenneth Petty na ametoa ishara kwamba anapanga kufunga naye ndoa.

Mbali na muziki , msanii huyo mwenye umri wa miaka 36 ameshiriki katika filamu kadhaa za Hollywood na anamiliki kipindi chake cha redio.

Hajasema anastaafu katika vitengo gani vya biashara yake na iwapo ni kweli.

Baada ya kuachilia vibao kadhaa katika miaka ya 2000 , Nicki Minaj alijiunga na Drake katika kampuni ya kurekodi muziki ya Lil Wayne Young Money Entertainment.

Albamu yake ya kwanza kwa jina Pink Friday ilitolewa 2010.

Nyimbo maarufu kama Super Bass, Anaconda na Starships zilimuimarisha kuwa mmojawapo wa marapa maarufu wa kike duniani.

Albamu yake ya pekee iliuza sana na ushirikiano wake na wasanii kama vile Ludacris, Usher, David Guetta, Madonna, Ariana Grande, Kanye West , Justin Bieber na wengine wengi bora.

Nicki Minaj akibeba tuzo aliyoshindaHaki miliki ya picha GETTY IMAGES

Ameteuliwa kushinda tuzo 10 za Grammy , akishinda tuzo 5 za MTV kwa kuwa na video bora na kuvunja rekodi ya Billborad kwa kushiriki mara 100 miongoni mwa msanii mmoja.

Mbali na Muziki , alishiriki katika filamu kama vile The Other Woman na Ice Age: Continental Drift.

line

‘Amekuwa akitaka kuwafungulia wengine milango’

Sinead Garvan, Ripota wa burudani wa Radio 1 Newsbeat anasema

Inaonekana kwamba neno kustaafu limetokea ghafla na hivyobasi kuwafanya wengi kusambaza uvumi kwamba Nicki Minaj sio mkweli.

Hatokuwa msanii wa kwanza kustaafu mapema- Jay-Z alifanya uamuzi kama huo 2003 na kufikia sasa ametoa vibao vitano naye Eminem akifanya kama hivyo.

Lakini ukichunguza kipindi cha muziki wa Nicki , amekuwa akionyesha hamu ya kutaka kuanza familia na kustaafu katika mambo tofauti.

Amekuwa akitaka kuwafungulia milango wasanii wengine wanawake ili kutawala – na amefanikiwa kufanya hivyo kufuatia kuwasili kwa Cardi B na Megan Thee Stalliuon.

Lakini pengine ushindani umeanza kuwa mkali dhidi yake.

Nicki hajawahi kushinda tuzo ya Grammy lakini Cardi B alishinda albamu ya rap ya mwaka kupitia Invasion of Privacy.

Nicki kwa sasa hana umaarufu mkubwa na kwamba amekuwa akishindwa na wasanii chipukizi na kwamba hilo huenda ndio linalomkera zaidi.

Ameendelea kukosoa sekta ya muziki . Hivyobasi pengine anachukua muda kustaafu kabla ya kurudi

line

Albamu yake ya nne Queen ilishindwa kuwa juu ya chati za muziki marekani hatua iliomfanya kukosoa kila kitu kutoka Spotify , hadi Travis Scott ambaye albamu yake ya Astroworld ilichukua nambari moja.

Baadaye alifutilia mbali ziara yake ya Marekani kaskazini.

Nicki MinajHaki miliki ya picha GETTY IMAGES

Alisema kwamba hana muda wa kufanya mazoezi ili kutoa kiwango cha tamasha anachotaka kutoa .

Lakini kulikuwa na thibitisho la mauzo ya chini ya tiketi ya tamasha hilo.

Alitoa wimbo mpya mwezi Juni na kwamba pia alikuwa akiifanyia kazi albamu yake mpya.

Kwa nyota ambaye anajulikana kwa taarifa za ujasiri, wakati mwingine zinazokinzana- hakuna ushahidi kwamba ataheshimu aliyoyasema.

Lakini inaweza kuwa kweli kwani kulikuwa na uvumi kwamba tayari alikuwa amefunga ndoa na Kenneth Petty kwa siri.

Newsbeat imewasiliana na kampuni yake ya kurekodi muziki lakini haijatoa tamko lolote.