Mti mrefu zaidi duniani wagunduliwa Asia

Nipashe Online: Wanasayansi nchini Uingereza na Malaysia wamegundua mti mrefu zaidi duniani ulio na urefu wa zaidi ya mita 100 au futi 328.

Mti huo uligunduliwa kwenye msitu wa Borneo huko Asia na kundi la wanasayansi kutoka chuo cha Nottingham mwaka uliopita.

Watafiti kutoka chuo cha Oxford kisha wakatumia teknolojia ya 3D na ndege zisizo na rubani kuthibitisha rekodi hiyo.

Mti huo uliogunduliwa katika bonde la Danum na kupewa jina Menara likimaanisha jengo refu.