Meneja wa Crystal Palace apigwa kalamu

Meneja wa Crystal Palace amepigwa kalamu na klabu hiyo baada ya kuongoza michezo mitano.

De boer ameongoza klabu hiyo kwa siku 77 pekee.

Meneja wa zamani wa England Roy Hodgson atachukua nafasi yake, BBC Sports imeeelezewa.

The Eagles wako katika nafasi ya 19 katika ligi ya Premia kwa kupoteza kwa Burnley 1-0 siku ya Jumapili. Crystal ilishindwa kufunga bao lolote latika mechi zao nne za ligi chini ya meneja De boer.

Meneja huyo wa zamani wa Ajax , De Boer , 47 alichukua kazi hiyo ya umeneja mwanzoni mwa msimu huu, baada ya Sam Allardyce aliyeiaga timu hiyo baada ya kuwaepesha katika hatua ya kushushwa daraja msimu uliopita.