Mbwa mwitu hupiga chafya kama kura wanapo amua kufanya jambo

Mbwa mwitu hufanya maamuzi yao kwa kupiga kura kupitia kupiga chafya kwa mujibu wa utafiti mpya.

Utafiti huo wa pamoja uliofanywa na wasomi kutoka Swansea, Australia na Marekani ulifuatilia mbwa mwitu walio kwenye hatari ya kuangamia nchini Botswana.

Waligundua kuwa mbwa walitumia chafya kuamua wakati wanaelekea kuwinda baada ya kufanya mikutano inayofahamika kuwa mikutano wa kijamii.

Awali ilikuwa ikifikiriwa kuwa mbwa hao ambayo ni familia ya wanyama walio kwenye hatari zaidi ya kuangamia duniani, walikuwa wakipiga chafya ya kawaida.

Lakini wakati watafiti walirekodi mikutano 68 ya mwa mwitu waligundua kuwa wakati walipiga chafya zaidi walikuwa wakiondoka na kuanza wa kuwinda.

Dr King anasema kuwa chafya hiyo ni lazima ifike kiwango fulani kabla ya wao kuamua kufanya kitu.

Pia uutafiti huo uligundua baadhi ya chafya huwa na uzito kuliko zingine.