Marekani kuwapeleka tena wanasayansi mwezini ndani ya miaka mitano

Makamu wa rais wa Marekani Mike Pence ametangaza lengo la haraka la kuwapeleka wamarekani mwezini tena, ndani ya miaka mitano “kwa nja yoyote ile,” ambapo afisa wa cheo cha juu wa NASA mara moja alikaribisha changamoto hiyo.

Pence alikuwa akiongoza mkutano wa barala za kitaifa la anga za mbali huko Alabama ambapo alisema ‘leo tuko katika mashindano ya anga za mbali jinsi tulivyokuwa miaka ya 1960.”

Kuwa na lengo kama hilo ambalo linatarajiwa kugharimu mabilioni ya dola linakuja wakati NASA inakumbwa na changamoto ikisaidiwa na kampuni za kibinafsi kurejea katika safari za naga za mbali kutoka ardhi ya Marekani kwa mara ya kwanza tangu shrika la NASA lisitishe programu zake mwaka 2011.

Lengo hilo la kufika mwezini linaashiria mpango wa Rais Doanld Trump kwa mipango mioya ya serikali wakati anataka kuchaguliwa tena huku akitaka kukabiliana uwezekano wa kuwepo kwa silaha za anga za mbali kutoka Urusi na China.

Awali NASA ilikuwa na lengo la kurejesha wanasayansi wake kwenye ardhi ya mwezi ifikapo mwaka 2028 baada ya kuweka kituo cha kupitia wanasayansi huko Orbit ifikapo mwaka 2024.