Majengo ya kisasa kutatiza maisha ya popo

Majengo ya kisasa yaliyo na vioo vikubwa au sakafu zenye vioo yamegunduliwa kuwa hatari sana kwa popo.

Wanasayansi wametaka hatari zilizopo kutiliwa maanani hasa maeneo ambapo popo hukusanyika kwa idadi kubwa.

Popo wana uwezo wa kuruka kwa kasi gizani na kujizua kukaribia vitu kama miti

Lakini maeneo yaliyo laini kama vile madirisha ya vioo husababisha popo kutoyatambua maeneo hayo.

“tuligundua kuwa popo wanaweza kutambua kimakosa maeneo lakini kama madirisha ya vioo kama yaliyo salama kupita na mara nyingi hugonga maeneo hayo.”