Mahakama yawazuia viongozi wa Chadema kusafiri nje ya nchi

Nipashe Online: Hakimu mkazi wa mahakama ya Kisutu amekataa maombi ya kusafri nje ya maafisa wawili wa Chadema, limeripoti gazeti la The Citizen nchini humo.

Maafisa hao wawili wanaokabiliwa na mashtaka katika mahakama hiyo ni Katibu Mkuu wa Chama Dkt Vicent Mashinji na mbunge wa Tarime Mjini Esther Matiko.

Wawili hao, kupitia mawakili wao walikuwa wameomba mahakama iwaruhusu wasafiri nje ya nchi kushiriki mkutano.

Dkt Masinji, Bi Matiko na viongozi wengine wa ngazi ya juu wanakabiliwa na mashtaka ya uasi katika mahakama hiyo.

Jumanne Septemba 24, 2019 kupitia wakili wao Profesa Abdallah Safari waliiomba mahakama kuahirisha kesi dhidi yao ili kuwaruhusu wasafiri ng’ambo.

Dkt Safari aliiambia mahakama kwamba Dkt Masinji anatakiwa kusafiri kuelekea London Uingereza tarehe 26 septemba mwaka huu , ambako alitakiwa kuhudhuria mkutano tarehe 6 Oktoba.

Wafuasi wa ChademaHaki miliki ya picha GETTY IMAGES-Wafuasi wa Chadema

Kwa upande mwingine , Bi Matiko alitakiwa kusafiri kuelekea Kigali Rwanda Septemba 25 ana baadae kwenda mjini Brussels, Ubelgiji kuhudhuria mkutano kati ya tarehe 13 na 18 Oktoba mwaka huu.

Akitoa hukumu juu ombi hilo hakimu Thomas Simba, alisema kuwa kutokana na kwamba mahakama imebaini kuwa washtakiwa wanakesi ya kujibu ,kuwaruhusu kusafiri kutachelewesha mchakato wa kesi hiyo.

“Washtakiwa wanapaswa kuanza kujitetea juu ya mashtaka yanayowakabili, kwa hiyo kwa kuwaruhusu wasafiri itachelewesha kesi ,” alisema Bwana Simba.

Aliamua kuahirisha kesi hadi tarehe 7 Oktoba , wakati upande wa washtakiwa utakapoanza kujitetea kwa siku tano mfulurizo.

Septemba 12, mahakama iliwapata na kesi ya kujibu maafisa tisa wa ngazi ya juu wa Chadema akiwemo mwenyekiti wa chama hicho ngazi ya taifa Freeman Mbowe.

Viongozi wa Chadema walianza kujitetea tarehe 17 mwezi SeptembaHaki miliki ya picha MWANANCHI-Viongozi wa Chadema walianza kujitetea tarehe 17 mwezi Septemba

Wanakabiliwa na kesi ya uhalifu , yenye makosa 13 ukiwemo uasi.

Uamuzi huo ulitolewa baada ya waendeshamashtaka kukamishi utoaji wa ushahidi wao dhidi ya washtakiwa.

Hakimu Simba alisema kuwa kwa kuzingatia ushahidi uliowasilishwa na mashahidi wa upande wa uendeshamashtaka na nyaraka nyingine zilizowasilishwa mahakamani anaamini kuwa washtakiwa wote wana kesi ya kujibu.

Miongoni mwa mashahidi wa upande wa uendeshamashtaka katika kesi hii pamoja na mkuu wa upelelezi kutoka Wilaya ya Kipolisi ya Mbagala, Bernard Nyambari 42 ), ambaye alieleza mahakama hiyo kuwa hotuba zilizotolewa na viongozi wa Chadema katika mkutano wa kufunga kampeni ya uchaguzi mdogo wa ubunge Kinondoni, zilizofanyika katika viwanja vya Buibui ndio chanzo cha wananchi kuandamana.

Mwaka 2018 viongozi hao waliwahi kuweka katika gereza la Segerea baada ya hakimu mkazi kuwaondolea dhamana:

Sambamba na Bwana Mbowe washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni pamoja na mbunge wa Tarime mjini , Esther Matiko; Mbunge wa iringa mjini , Peter Msigwa; Naibu Katibu mkuu- Zanzibar, Salum Mwalimu; mbunge wa Kibamba , John Mnyika; mbunge wa Kawe Halima Mdee, mbunge wa Tarime vijijini , John Heche, Mbunge wa Bunda , Ester Bulaya na Katibu Mkuu wa Chadema Dkt. Vicent Mashinji.

Washtakiwa kujitetea Septemba 17, na wote wako nje kwa dhamana.