Kampuni ya Google – Loon kutumia puto kutoa mtandao Kenya

Puto kadhaa hivi karibuni zitaanza kuwapa watu huduma ya mtandao sehemu za mashambani nchini Kenya.

Kampuni ya Google – Loon, imetangaza ushirikiano wake wa kwanza na kampuni ya mawasiliano nchini Kenya Telkom kupeleka huduma ya mtandao maeneo hayo.

Puto zenye mitambo maalum ya kusambaza mitandao zitapaa kwenye anga tofauti za nchi hiyo ya Afrika mashariki.

Mtandao huu uliokuwa ukifahamika kama Project Loon, teknolojia yake iliundwa na kampuni mzazi inayofahamika kama Alphabet.

Mapema mwezi huu kampuni hiyo ilipanuka na kuwa kampuni inayojisimamia.