Jinsi wanasayansi wanavyolenga kudukua ubongo wa mwanadamu

Nipashe Online: NeuraLink, kampuni ilioanzishwa na Elon Musk ili kutafuta mbinu za kuunganisha ubongo wa mwanadamu na tarakilishi imewasilisha ombi kwa wadhibiti wa Marekani kuanza kupima kifaa chake miongoni mw awanadamu.

Mfumo huo umejaribiwa katika tumbili ambaye aliweza kudhibiti tarakilishi na ubongo wake kulingana na bwana Musk.

Kampuni hyo ilikuwa inalenga kuwaangazia wagonjwa wenye matatizo ya uti wa mgongo, neva na ubongomiongoni mwa binadamu.

Lakini hatahivyo lengo la bwana Musk ni kudukua ubongo wa mwanadamu kupitia tarakilishi.

Kushirikisha ubongo wa mwanadamu na ule wa mashine

Kifaa ambacho kampuni imetengeneza kina kifaa kidogo kinachoweza kuchunguza- chenye electrodes zaidi ya 3,000 zilizounganishwa na nyuzi zinazoweza kubadilika – ambazo ni nyembamba kuliko nywele za binadamu – na ambazo pia zinaweza kufuatilia shughuli za neuroni 1,000.

Umuhimu wa mfumo huo, kulingana na kampuni hiyo ni kulenga maaneo fulani katika ubongo hatuaainayofanya upasuaji kuwa salama.

CPU Mind series. Backdrop composed of human face silhouette and technology symbols and suitable for use in the projects on computer science, artificial intelligence and communications

Pia kinaweza kutathmini yaliorekodiwa kupitia mashine ambayo itaamua ni aina gani ya matibabu yatakayopewa mgonjwa.

Neuralink hatahivyo haikutoa maelezo jinsi mfumo huo unavyoweza kubadilisha vitendo vya ubongo ama jinsi kifaa hicho kilivyoweza kuchochea seli za ubongo.

”Sio kwamba tayari tutakuwa tuna uwezo wa kushirikisha ubongo wa mwanadamu katika tarakilishi na kuchukua udhibiti wa bongo za wanadamu”, alisema bwana Musk.

Hiki ni kitu kitakachochukua muda mrefu. Lakini alisema kwamba wale watakaotaka kutumia mfumo huo utasaidiana na ule wa tarakilishi.

Awali Bwana Musk alikuwa amesema kuwa inteligensia ya mashine inaweza kuharibu jamii ya wanadamu.

Uunganishaji wa ubongo na tarakilishi utaimarisha zaidi ubongo wa mwanadamu , alisema akiongezea kwamba tayari watu wamekuwa wakifurahia hilo kupitia simu zao.

Baadaye baada ya muda wa maswali na majibu , alifichua kwamba kifaa hicho cha Neuralink kinafanya kazi na kwamba tayari kimefanyiwa vipimo katika tumbili huku mnyama huyo akiweza kudhibiti tarakilishi na ubongo wake , Kulingana na bwana Musk.

Sasa kampuni hiyo imewasilisha ombi la kutaka kuwajaribu wanadamu na mfmo huo ambalo litahitajika kuidhinishwa na kitengo cha usimamizi wa chakula na dawa nchini Marekani.

Bwana Musk pia analenga kuajri mwanasayansi mmoja zaidi katika kampuni hiyo ambayo kufikia sasa inaendeshwa na wafanyikazi 100.

Ubongo uliounganishwa na tarakilishiHaki miliki ya picha GETTY IMAGES

Mpango wa kudukua ubongo wa mwanadamu- kampuni hiyo inasema utachukua miaka mingi ya kazi kufanywa ili kukabiliana na changomoto za kiteknolojia pamoja na kimaadili, lakini teknolojia hiyo huenda ikawa hatua kubwa katika kukabiliana na matatizo sugu ya kiafya kama vile ugonjwa wa kifafa na ule wa kutetemeka.

Miradi mingi ya bwana Musk inajaribu kufanya yale yanayowezekana.

Mradi wa Space X unalenga kuanzisha utalii wa kuelekea sayari ya Mars huku kampuni ya Boring ikijaribu kujenga mahandaki chini ya mji wa Los Angeles huku mradi wake wa Hyperloop ukilenga kuimarisha usafiri kwa njia nyengine.