Jinsi rubani aliyekuwa anavuta sigara alisababisha ndege ishuke ghafla

Rubani msaidizi ambaye alikuwa anavuta sigara ndani ya ndege ya shirika la Air China, alisababisha ndege hiyo kuanza kushuka ghafla, kwa mujibu wa uchunguzi uliofanyiwa.

Wachunguzi wanasema alijaribu kuficha ukweli kuwa alikuwa anavuta sigara la kwa bahati mbaya akazima mitambo ya hewa hatua iliyosababisha viwango vya Oxygen kushuka ndani ya ndege.

Ndege hiyo iliyokuwa safarini kutoka Hong Kong kwenda mji wa Dalian iliachilia vifaa vya kupumua na ndege yenyewe ikashuka chini mita 6,500.

Lakini baadaye ilireja eneo lake la kawaida na kuendelea na safari.

Uchunguzi ulionyesha kuwa rubani msaidizi alijaribu kuzima mitambo ya hewa kuzuia moshi wa sigara kuwafikia abiria bila la kumjulisha rubani mkuu, lakini badala yake akaizima kwa bahati mbaya mitambo tofauti ya kudhibiti hewa ndani ya ndege.

Abiria wanasema waliambiwa wafunge mikanda kwa kuwa ndege ingeshuka.

Aircraft passengers with oxygen masks dropped