Jenerali wa ngazi ya juu wa Iran auawa na Marekani Iraq

Qasem Soleimani

Nipashe Online: Qasem Soleimani, Jenerali wa vikosi vya kikurdi vinavyoungwa mkono na Iran, ameuawa na vikosi vya Marekani nchini Iraq.

Pentagon imethibitisha kuwa aliuawa kufuatia “amri ya rais”.

Hayo yamejiri kufuatia ripoti ya mashambulio katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Baghdad, ambayo ilisema watu kadhaa wameuawa.

Waziri wa mambo ya nje wa Iran, Javad Zarif, ametaja hatua hiyo kuwa “hatari na uchokozi wa kishenzi”.

Gen. Soleimani alikuwa mtu mashuhuri kwa utawala wa Iran. Kikosi chake cha Kikurdi kilikuwa kinaripoti moja kwa moja kwa kiongozi mkuu wa kidini wa Iran Ayatollah Ali Khamenei na alisifiwa kama shujaa wa kitaifa.

Rais wa Marekani Donald Trump aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter picha ya bendera ya Marekani baada ya kutangazwa kuuawa kwa jenerali hiyo.

Bei ya mafuta duniani imepanda kwa asilimia nne baada ya shambulio hilo.

Nini kilichofanyika?

Ripoti za vyombo vya habari vya Marekani zinasema kuwa Jenerali Soleimani na maafisa wa waasi wanaoungwa mkono na Iran nwalikuwa wakiondoka katika uwanja wa ndege wa Baghdad kwa kutumia magari mawili wakati waliposhambuliwa na ndege za Marekani zisizokuwa na rubani karibu na eneo kuweka mizigo.

Kamanda huyo aliripotiwa kusafiri kutoka Lebanon au Syria. makombora kadhaa yaliripotiwa kushambulia msafara wao, ambapo karibu watu watano wanaaminiwa kuawa.

Taarifa iliyotolewa na Pentagon ilisema: “Kufuatia agizo la rais, vikosi vya jeshi la Marekani vilichukua hatua ya kuwalinda wafanyikazi wake nje ya nchi kwa kumuua Qasem Soleimani,”

“Hatua hii ililenga kudhibiti mipango ya Iran ya mashabulio ya siku zijazo. Marekani itaendelea kuchukua hatua madhubuti kuwalinda watu wetu na maslahi yetu kote duniani,” ripoti hiyo iliendelea kusema.

Shambulio hilo la ndege zisizo na rubani linakuja baada ya siku kadhaa za maandamano ambapo waandamaanaji waliokuwa wakishambulia ubalozi wa Marekani mjini Baghdad kukabiliana na vikosi vya Marekani katika eneo hilo.

Pentagon inasema jenerali Soleimani aliidhinisha mashambulio dhidi ya ubalozi wa Marekani.

Kikosi maalum cha jeshi la Iran kimesema kiongozi wa waasi wa Iraq Abu Mahdi al-Muhandis pia ameuawa katika shambulio hilo lililotekelezwa na Marekani, na kulaumu mashambulio ya helikopta kutoka kwa nchi hiyo.

Ripoti zinaashiria kuwa viongizi kadhaa wa waasi wa Iraq wanazuiliwa na vikosi vya Marekani mjini Baghdad, japo tarifa hizo hazijathibitishwa.

Qasem Soleimani ni nani?

  • Tangu mwaka Since 1998, Meja Jenerali Qasem Soleimani ameongoza vikosi vya kikurdi nchini Iran- kengo maalum cha jeshi la Iran (Revolutionary Guards) ambacho huendesha opareshani zake nje ya nchi.
  • Alikuwa kiungo muhimu katika mapambano ya kimkakati mashariki ya kati kupitia vikosi vya Kikurdi, ambavyo vinaendesha oparesheni yake kwa ushirikiano na jeshi la ulinzi la Iran.
  • Meja jenerali Qasem Soleimani, na vikosi vyake vinafanya kazi chini ya kiongozi mkuu wa kidini, Ayatollah Ali Khamanei, badala ya kufuata muundo wa kawaida wa kijeshi wa Iran.
  • Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo alitaja jeshi la ulinzi la Iran Revolutionary Guards na washirika wake vikosi vua Kikurdi kama shirika la kigeni la ugaidi mwezi April mwaka jana.