India: Kijiji kilichozama kinachoonekana mwezi mmoja kwa mwaka

Bwawa la kwanza la jimbo hilo lilizamisha kijiji cha Curdi

Nipashe Online: Kijiji cha kimoja magharibi mwa India kinaonekana kwa mwezi mmoja – miezi 11 iliyosalia, kijiji hicho huzama chini ya maji.

Maji yanapokauka, wakaazi wake waliyohamishwa katika sehemu nyingine, huja pamoja kusherehekea ujio wa kijiji chao, Supriya Vohra anaripoti.

Kijiji cha Curdi kinapatikana katikati ya milima miwili ya magharibi ya Ghats na mto Salaulim river – moja ya mito mikubwa katika jimbo la Goa.

Kijiji hicho wakati mmoja kilikuwa kimeendelea sana na kilikuwa maarufu sana katika jimbo hilo.

Mwaka 1986, Bwawa la kwanza lilijengwa katika la jimbo hilo na matokeo yake ilikuwa kuzama kwa kijiji hicho.

Lakini kila mwaka mwezi Mei, maji yakipungua mabaki ya kijiji hicho huonekana.

Ardhi iliyopasuka, mabaki ya mijengo iliyokuwepo na vifaa vya nyumba vilivyovinjika huonekana katika eneo hilo.

Curdi
Wakati mmoja kijiji cha Curdi, kilikuwa kimeendelea

Ardhi katika eneo hilo ilikuwa na rutuba kuliko ardhi zingine katika vijiji vya karibu, na kilitegemewa na watu karibu 3,000- ambao walilima nazi, korosho, maembe na matunda mwengine.

Waumini wa Kihindu, Waislamu na Wakristo wamekuwa wakijumuika pamoja katika maeneo ya ibada, kufanya ibada maalum.

Lakini mambo yalibadilika baada ya Goa kupata uhuru wake kutoka kwa Wareno mwaka 1961.

Waziri kiongozi wa kwanza, Dayanand Bandodkar, alizuru kijiji hicho na kutangaza mpango wa ujenzi wa bwawa la kwanza katika jimbo hilo.

Alu=iwaleta pamoja wakaazi wote na kuwaelezea manufaa ya ya bwawa hilo kwa watu wote wa kusini mwa Goa.

Curdi
Maji yanapopungua kila mwaka mabaki ya kijiji hicho huonekana

“Alisema itazamisha kijiji chetu lakini ni hatua itakayoleta manufaa makubwa kwetu sote,”Mzee Gajanan Kurdikar, wa miaka 75 alisimulia kumbukumbu yake kuhusu mkutano huo.

Bw. Kurdikar na wakaazi wengine, wanaojumuisha familia 600, walilazimika kuhamia vijiji vingine karibu na hapo baada ya kufidiwa kwa ardhi nyingine .

Mradi wa ujenzi wa bwawa hilo ulifanywa katika kingo za mto Salaulim, na ulipewa jina la kilimo cha unyunyuziaji maji cha Salaulim.

Ulipendekeza kuwa utaleta maji ya kunywa, kilimo na viwanda katika maeneo ya kusini mwa Goa. Na ulilenga kuwasidiawakaazi na lita milioni 400 ya maji kila siku.

“Tulipohama katika kijiji kipya hapakuwa na lolote,” anakumbuka Inacio Rodrigues. Alikuwa miongoni mwa familia za kwanza zilizohama mwaka1982.

Walilazimika kukaa katika makaazi ya mudu hadi walipo jengwa nyumba zao na wengine iliwachukua hadi miaka mitano.

Bwawa la Salaulim
Bwawa la kwanza la maji lilijengwa kuwapa maji wakaazi wote wa kusini mwa Goa

Gurucharan Kurdikar alikuwa na miaka 10 wakati familia yake ilipohamia kijiji kipya mwaka 1986.

“Nakumbuka wazazi wangu waliharakisha kuweka vitu katika gari, nikaambiwa niingie, tukawachukua ndugu yangu na bibi yangu njiani na kuondoka.

Wazazi wangu walitufuata baadae,” anakumbuka bwana huyo wa miaka 42.

Mama yake Mamta Kurdikar, anakumbuka siku vizuri sana. “Nakumbuka tulikuwa familia za mwisho kuhama. Kulinyesha sana siku moja kabla ya sisi kuondoka, na maji kutoka maeneo ya mashambani yalianza kuingia majumbani. Tulilazimika kuondoka mara moja. Si kuweza hata kubeba mtambo wangu wa kusaga unga,” alisema.

Gajanan na Mamta Kurdikar
Gajanan na Mamta Kurdikar sasa wanaishi katika kijiji cha Vaddem

Lakini maji kutoka kwa bwawa hilo hayakufika katika vijiji vilivyohamiwa na wakaazi wa Curdi.

“mfumo wa mabomba ya maji haukuwafikia wakaazi wa kusini mwa Goa kama walivyoahidiwa,” Gajanan Kurdikar anasema. “Kwahivyo hatupati maji ya kunywa kutoka kwa bwawa hilo.”

Katika kijiji cha Vaddem, ambako Bw. Kurdikar anaishi sasa kuna visima viwili vikubwa vya maji. Lakini visima hivyo huanza kukauka mwezi wa Aprili na ikifika Mei, hukauka kabisa.

Wanalazimika kutegemea maji ya kunywa kutoka kwa serikali.

Maji yanapokauka mwezi mei wakaazi asilia wa kijiji cha Curdi huzurimaeneo hayo.

Curdi
Karibu wakaazi 3,000 waliishi katika kiji cha Curdi kabla walazimishwe kuhama