Ifahamu nchi inayotarajiwa kuwa tajiri zaidi duniani

Nipashe Online: Nchi ya pili kwa umasikini Amerika ya kusini imeanza ujenzi wa bomba la mafuta ambalo linaweza kuifanya nchi hiyo kuingia katika idadi ya nchi tajiri zaidi katika bara hilo na hata duniani.

Lakini Guyana inaweza kuepuka zile zinazotajwa kuwa laana za utajiri wa mafuta na kuhakikisha kuwa rasilimali hiyo mpya itaweza kuwanufaisha kila mwananchi wa Guyana.

“Watu wengi hawaelewi mradi huu ni mkubwa kiasi gani”, balozi wa Marekani nchini Guyana ,Perry Holloway alisema hayo katika mji mkuu wa Georgetown,mwezi Novemba.

GAYANA

Mwaka 2020, pato la ndani liliongezeka kutoka asilimia 300 mpaka 1000. Hatua hiiyo ni kubwa . Nchi hii inaweza kuwa na utajiri wa nusu ya nchi zote zinazotajwa kuwa ni nchi tajiri zaidi ”

Jambo hili linaweza kuonekana kuwa ni la kusadikika lakini katika idadi ya watu wapatao 750,000, utajiri wa Guyana umebuniwa kuwa juu.

ExxonMobil, ambao ni waendeshaji wakuu wa mradi huo huko Guyana wanasema kuwa wamebaini zaidi ya mabomba bilioni 5.5 ambayo yana thamani sawa na mafuta ambayo yako chini ya maji katika bahari ya Atlantiki.

‘Laana ya mafuta’

Fedha ambazo zitakuja , katika koloni hili la zamani la Uingereza huko Amerika ya kusini kuna idadi kubwa ya watu ambao hawana ajira na kiwango cha umasikini kiko juu.

Lakini historia inawapa tahadhari Guyana . Kupatikana huku kwa rasilimali kubwa ya mafuta katika nchi nyingine zilizoendelea zimekabiliwa na rushwa ya kiwango cha juu na hivyo kupelekea utajiri huo kupotea na kuibiwa. Ndio maana utajiri huo ukafahamika kuwa ni laana ya mafuta.

Troy Thomas kiongozi wa taasisi ya kimataifa ya kutokomeza rushwa
Troy Thomas kiongozi wa taasisi ya kimataifa ya kutokomeza rushwa

Guyana, “Rushwa ipo sana” alisema Troy Thomas kiongozi wa taasisi ya kimataifa ya kutokomeza rushwa. Kiongozi huyo alisema kuwa ana hofu juu ya laana ya mafuta. Changamoto za kisiasa katika miezi ya hivi karibuni imeonekana na baadhi kuwa ni dalili za awali za athari za laana hiyo.

Baada ya serikali ya muungano kupoteza kura ya kutoaminika mnamo mwezi Desemba, na badala yake kutaka uchaguzi, ambao kura zake zitashindaniwa mahakamani.

Jambo ambalo lilisababisha maandamano.

” Kile ambacho tunakitaka serikali ifanye ni kuheshimu katiba yetu , mmoja wa waandamanaji alisema wakati akiwa amesimama nje ya ofisi ya wizara inayoshughulikia masuala ya rais , “Hawa wanataka kubaki na utawala na kuzithibiti fedha zote za mafuta” aliongeza dada huyo.

Mapambano ya kisheria yanaendelea na wiki hii Mahakama ya Haki ya Caribbean inatarajia kusikiliza rufaa ya mwishi ya kesi hiyo.

Kupambania elimu

Vincent Adams
Vincent Adams

“Tumeona jinsi nchi nyingine zilipopitia” , alisema Vincent Adams ambaye ni kiongozi mpya wa Guyana katika masuala ya usalama wa mazingira, na aliwahi kufanya kazi katika idara ya nishati nchini Marekani.

” Wamepata utajiri wa mafuta yote haya nan chi nyingine nyingi ambazo zilifanikiwa kupata utajiri wa namna hii wako kwenye hali mbaya zaidi ya walivyokuwa zamani kabla hawajapata mafuta .”

Jambo la muhimu ili kukabiliana na changamoto zinazoweza kutokea ni ” Elimu , elimu elimu ndio msingi, huo ndio msingi bora kabisa katika uwekezaji wa nchi hii au nchi nyingine yeyote.”