Griezmann afungua ukurasa wake wa magoli katika Barcelona

Nipashe Online: Mshambuliaji wa Barcelona Antoine Griezmann amefungua rasmi ukurasa wa magoli ndani ya timu hiyo kwenye Ligi Kuu ya Hispania dhidi ya Real Betis katika ushindi wa magoli 5-2.

Griezmann alifungua ukurasa wa magoli kunako dakika ya 41 na 50, wakati magoli mengine yakifungwa na Carles Pérez kunako dakika ya 56, Jordi Alba 60 na Arturo Vidal 77.

Upande wa Betis walianza kwa kufunga goli dakika ya 15 kupitia ingizo jipya la Nabil Fekir, kisha wakati wa
magharibi ya roho wakafunga goli lingine na Morón dakika ya 79.

Griezmann, ambaye alijiunga na Barcelona Julai kwa dau la pauni milioni 107 alifunga goli la kwanza akisawazisha
goli la mapema la Fekir.

Mshambuliaji huyo raia wa Ufaransa alikuwa kwenye hofu kubwa kutokana na kushindwa kuonyesha ubora mkubwa
sawa na mategemeo ya mashabiki wengi, magoli hayo yanafuta fununu za kufuata nyayo za Courtinho.

Matokeo hayo yanaifanya FC Barcelona kufikisha alama tatu katika michezo miwili ambayo imecheza ya La Liga
huku idadi kubwa ya majeraha ikiendelea kuikumba timu hiyo.

REKODI

Kinda Ansu Fati, 16 na siku 298 ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa pili mdogo zaidi kuichezea FC Barcelona
katika umri huo wakati ambapo bado rekodi imezidi kushikiliwa na Vicente Martinez aliyecheza mechi yake ya
kwanza akiwa na miaka 16 na siku 280 dhidi ya Real Madrid mwaka 1941.

Mwandishi: Bruce Amani