Fuvu la binadamu wa kale mwerevu lagunduliwa

Fuvu hili lilikuwa na ubongo mdogo na sura ukilinganisha na binadamu wa sasa

Nipashe Online: Watafiti wamebaini fuvu la binadamu wa kale lililoishi zaidi ya miaka milioni 3.8 huko nchini Ethiopia.

Utafiti huo unatoa changamoto mpya kuhusu binadamu wa kale walivyokuwa wanaishi .

Hali ya sasa inaonyesha namna ambavyo fuvu la binadamu wa kale lililojulikana kama Lucy kuwa ndio lilidhaniwa kuwa ndio binadamu wa kwanza.

Utafiti huo uliripotiwa na jarida la ‘Nature’.

Fuvu hilo liligunduliwa na profesa Yohannes Haile-Selassie katika eneo linanaloitwa Miro Dora, katika kitongoji cha Mille huko nchini Ethiopia.

Mwanasayansi, ambaye alikuwa anafanya kazi katika nyumba ya makumbusho ya kihistoria Cleveland iliyopo Ohio nchini Marekani aligundua haraka umuhimu wa mabaki hayo .

“Nilijifikiria mwenyewe kwanza, ‘ ooh Mungu wangu – Je ninakiona kile ninachokifikiria kuwa ninakiona?’. Mara ghafla tu niliruka ruka kwa furaha na kuamini kuwa nilikuwa sioti bali hiyo ni hali halisi,” Mtafiti huyo aliiambia BBC.

Profesa Haile-Selassie anasema kuwa masalio hayo ni mifano mizuri ya binadamu wa kale kama vile fuvu la Australopithecus anamensis – ambalo linadhaniwa kuishi miaka mingi kama milooni 4.2 iliyopita,

Ilidhaniwa kuwa Aanamensisndio alikuwa binadamu wa kale zaidi, baadae yakapaikana masalio yalioendelea zaidi yalioitwa Australopithecus afarensis,ambayo baadae masalio hayo yalitajwa kuwa kuwa ni ya binadamu wa kale mwenye akili zaidi aliyewahi kuishi aliyejuliakana kama Homo, ambaye alijumuisha binadau wote wanaoishi hii leo.

Four views on the nearly complete skullHaki miliki ya picha CLEVELAND MUSEUM OF NATURAL HISTORY-Picha tofauti tofauti za muonekano wa fuvu jipya la binadamu wa kale.

Fuvu la mwili wa binadamu kwanza liligunduliwa mwaka 1974 . Watafiti walilipa fuvu hilo jina la utani kuwa ni Lucy baada ya wimbo uliovuma wa Lucy akiwa angani na almasi(Lucy in the Sky With Diamonds).

Hailed alisema kuwa Lucy alikuwa binadamu wa kale wa kwanza kutembea na hivyo kuvuta hisia za wengi.

Na kwa sababu hiyo binadamu wa kale la anamensis naafarensis‘ waliishi miaka iliyokaribiana.

Na sasa ndio imegundulika kuwa masalia ya binadamu hao wa kale yameishi kwa miaka takribani 100,000.

Kile ambacho kilitokea kilikuwa katika kundi dogo la anamensiskujitenga lenyewe katika idadi kubwa ya watu kulingana na muda kutokana na kuendana na mazingira halisi.

Matokeo ya utafiti huo yalikuwa muhimu kwa sababu yalionyesha tofauti na masalio mengine ya binadamu wa kale yalioonekana, na kuonyesha utofauti wa binadamu hao wa kwanza.

Ugunduzi huu mpya haukatai kuwa Lucy alikuwa binadamu wa kale wa kwanza kuwa mwerevu na wengine kutokubalika.

LucyHaki miliki ya picha P.PLAILLY/E.DAYNES/SPL-Mabaki ya binadamu wa kale ya Lucy yalidhaniwa kuwa ni ya binadamu wa kwanza
Presentational white space

Anamensis ni binadamu wa kale aliyegunduliwa hivi karibuni ambaye alionyesha kuwa hakukuwa na mstari ulionyooka wa binadamu wa kale mpaka binadamu wa sasa.

Ukweli bado unachanganya na bado unavutia zaidi.

Uvumbuzi huu unaeleza mzunguko wa ukuaji watu mbalimbali katika maeneo tofauti tofauti jinsi walivyokuwa werevu katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, chakula na harakati za maisha kwa ujuma.

Profesa Haile-Selassie ni miongoni mwa wanasayansi wachache wa Afrika ambao wanafanyia kazi historia ya binadamu wa kale.

Kwa sasa jina lake linajulikana lakini anasema si rahisi kwa watafiti wa Afrika kupata ufadhili kutoka nchi za magharibi katika taasisi zao.