CORONA: Amri ya kutotoka nje yatangazwa Nairobi na Mombasa

Waziri wa Afya Kenya Mutahi Kagwe

NIPASHE ONLINE: Wakaazi wa Maeneo ya Eastleigh jijini Nairobi na Old towm mjini Mombasa nchini Kenya hawatoruhusiwa kutoka katika maeneo hayo katika kipindi cha wiki mbili zijazo kuanzia saa moja usiku wa Jumatano Mei 6, 2020.

Hatua hiyo inalenga kuzuia kuenea kwa maambukizi ya virusi vya corona katika maeneo mengine ya miji ya Nairobi na Mombasa huku wagonjwa wengine wapya 47 wakitangazwa na kufanya idadi ya maambukizi kufikia watu 580.

Akizungumza na vyombo vya habari Waziri wa Afya Mutahi kagwe amesema kwamba kati ya wagonjwa hao 47, 32 wanatoka Mombasa huku 11 wakitoka Nairobi.

Amesema mtaa wa Bondeni ambao wakaazi wake wamekuwa wakiuka masharti ya afya yaliotolew na serikali una wagonjwa 18 wapya huku mtaa wa Estleigh ukiripoti wagonjwa 5 wapya.

Waziri Kagwe ameoonya mitaa mingine kwamba itachukuliwa hatua kama hiyo iwapo itaendelea kukiuka maagizo ya Kiafya na kusababisha maambukizi ya kiwango cha juu.

Waziri huyo pia ameagiza kwamba mikahawa iliopo katika maeneo hayo iendelee kufungwa wakati wa amri hiyo ya kutotoka nje.

Kagwe amesema kwamba wagonjwa 31 waliogunduliwa na ugonjwa huo ni wanaume huku 16 wakiwa wanawake.

Amesema kwamba watu wawili walifariki nyumbani kwao huko MOmbasa na kufanya idadi ya waliofariki kufikia 26. ”Iwapo kuna wagonjwa ambao wamefariki nyumbani huko Old Town hiyo inamaanisha kwamba kuna watu wengi wa familia waliopata maambukizi wakiwaangalia wagonjwa hao”

Wagonjwa wawili waliofariki nyumbani mjini Mombasa walikuwa na umri wa miaka 68 na 72 mtawalia.Wakati huo huo Serikali pia imesema kwamba italipia gharama za vituo vya karantini vinavyosimamiwa na serikali.

Gharama ya vituo vya karantini katika vifaa vya serikali zitalipwa na serikali, alisema kwagwe.

Hatua hiyo inaleta afueni kwa Wakenya wengi ambao wamelalamika dhidi ya kutakiwa kulipa ada za vifaa hivyo.

Kagwe pia ameripoti kwamba watu qwengine wanane wamepona ugonjwa huo , na kufanya idadi ya wale waliopona kufikia 190.

Ongezeko la visa vya maambukizi mapya katika kiswa cha Mombasa ni ishara kwamba virusi hivyo vimesambaa hadi katika mitaa yote.

Kupuuzwa kwa amri za serikal kuhusu kukabiliana na virusi hivyo hususan maagizi ya kutokaribiana uvaaji wa barakoa na uoashaji wa mikono mara kwa mara ndio sababu za kuene akwa virusi hivyo.Wiki iliopita waziri huyo alisema kwamba mitaa ya Nyali, Mvita na kisauni ndio mitaa ilioathirika pakubwa.

Hatua hiyo inajiri baada ya Gavana wa kaunti ya Mombasa Hassan Joho kuwahimiza wakaazi wa maeneo hayo kufuata maagizo hayo.

Joho amedai kwamba utamaduni na imani za kidini katika eneo hilo ndio sababu zinazosababisha kuenea kwa ugonjwa huo hususan wakati huu wa mwezi wa ramadhan ambapo wakaazi wengi hufanya ibada za pamoja na kufungua kwa pamoja.

Hatahivyo baadhi ya wakaazi wameonekana wakikaidi hadharani maagizo hayo ya kiafya na kuamua kufuangua pamoja baada ya kufunga mchana kutwa.