Boeing kupunguza uzalishaji wa ndege ya 737 baada ya ajali mbili

Nipashe Online: Boeing imesema ina mpango wa kupunguza uzalishaji wa ndege ya 737 kwa karibu assilimia 20 kwa mwezi baada ya ajali mbili za ndege, ikiwa ni ishara kuwa huenda mamlaka za safari za ndege zisiruhusu kutumika kwa ndege hiyo hivi karibuni.

Uzalishaji wa ndege hiyi bora zaidi ya Boeing unapungua kufuatia ajai iliyokumba shirika la ndege la Ethiopia Machi 10 na kuwaua watu 157.

Uzalishaji utapunguzwa hadi ndege 42  kwa mwezi kutoka ndege 52 kati kati ya mwezi Aprili kwa mujibu wa Boeing.

Marekani na maafisa wa shirika  hilo wanaamini huduma za ndege hizyi zitasitishwa kwa takriban miezi miwili lakini kuna uwezekano kuwa muda unaweza kuwa mrefu zaidi.

Ajali ya ndege hiyo nchini Ethiopia na ile ya Lio Air ya nchini Indonesia Oktoba iliyopita iliyowaua watu 189 imekuwa changamotio kubwa kwa kampuni hiyo kubwa zaidi duniani ya kuunda ndege.