Babu Tale Aanika Ukweli Kuhusu Rich Mavoko Kutimuliwa WCB

Meneja wa staa wa Bongo fleva na CEO wa WCB Diamond Platnumz, Babu Tale amefungukia kwa mara ya kwanza tetesi zinazoendelea kusambaa Kwenye mitandao ya kijamii kuwa Rich Mavoko katimuliwa.

Tetesi hizi zilianza wiki chache zilizopita baada ya Mavoko kutoonekana Kwenye tangazo jipya la Trailer ya Wasafi reality show lililowaonyesha wasanii wote wa WCB na familia ya Diamond.

Kwenye mahojiano Babu Tale alisema kwamba tetesi hizo siyo za kweli na Mavoko bado yupo WCB ila kipindi ambacho walikuwa wanachukua video ya Reality Show aliyoiposti Diamond ambayo ndiyo iliyozua maneno mwanamuziki huyo hakuwepo alikuwa kwao Mahenge, Morogoro kwenye msiba kwani alifiwa na dada yake.

Wakati tunarekodi hiyo video ya Reality Show, Mavoko alikuwa Mahenge kwao, alifiwa na dada yake kwa hiyo alikuwa kwenye msiba, lakini hizi siku zote yupo bize anashuti wimbo wake mpya na zamu inayokuja ni yake kuachia wimbo kwani sisi huwa tunaachiana muda wa kutoa nyimbo kwa hiyo sioni haja ya kuongopa kwamba hayupo WCB, kwa sababu hata asipokuwepo lazima itajulikana tu”.

Baada ya habari kuanza kusambaa Mavoko alimtafuta ili kuthibitisha taarifa hizo lakini alikataa kabisa kuongea na kutaka uongozi wake utoe majibu ya maswali hayo.