Athari ya Google kupiga marufuku Huawei kutumia huduma za Android

Nipashe Online: Google imepiga marufuku kampuni ya simu ya pili kubwa duniani, Huawei, kutumia baadhi ya huduma kutoka mfumo wa uimarishaji kazi ya simu – Android, hatua ilio pigo kubwa kwa kampuni hiyo ya China.

Aina mpya za simu za Huawei hazitoweza kutumia baadhi ya programu tumishi kutoka Google apps.

Hatua hiyo inajiri baada ya serikali ya Marekani kuiorodhesha Huawei katika makampuni ambayo ni marufuku kwa makampuni ya Marekani kushirikiana nayo ila tu wakiwa na kibali.

Google inasema “inafuata agizo hilo na kutathmini athari”.

Huawei imesema itaendelea kutoa mfumo wa kuimarisha matumizi ya simu zake na huduma za baada ya mauzo kwa bidhaa zote za simu, tabiti ambazo tayari zimeuzwa au zile ambazo zingali zinasubiri kuuzwa kote duniani.

“Tutaendelea kujenga mfumo salama na wa kudumu, ili kutoa huduma nzuri kwa wateja wote duniani,” imeendelea kuhakikisha.

Woman looking at Huawei phoneHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Ina maana gani kwa wamiliki simu za Huawei?

Maswali mengi yameulizwa kuhusu athari ya mvutano huu kwa wateja wa bidhaa za Huawei barani Afrika.

Katika mitandao ya kijamii kwa mfano watu wamekuwa wakifuatilia mvutano na taarifa kuhusu Google kupiga marufuku Huawei kutumia huduma za Android na athari yake kwa simu za Huawei ambazo baadhi tayari wanazitumia:

Wamiliki na watumiaji simu za Huawei wataweza kwa sasa kuimarisha programu tumishi na usalama wa simu zao pamoja na kuweza kuimarisha huduma ya Google Play.

Lakini Google itakapozindua aina mpya ya mfumo wa Android baadaye mwaka huu, huenda isipatikane kwenye simu, tabiti na vifaa vingine vya Huawei.

Vifaa vingine vya Huawei huenda visiwena programu tumishi kama YouTube na ramani yaani Google Maps.

Huawei bado inaweza kutumia mfumo wa ufanyaji kazi wa Android uliopo sasa kupitia kibali cha wazi.

Ben Wood, mtaalamiu wa mshauri wa masuala ya teknolojia, amesema hatua ya Google itakuwa na “athari kubwa kwa biashara ya Huawei”.

Huawei staff look at mobile firms at firm's campus in Shenzhen, China, 12 April 2019Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Huawei inaweza kulirekebisha vipi hili?

Huawei inakabiliwa na upinzani kutoka mataifaya magharibi, ikiongozwa na Marekani, kuhusu hatari inayowezekana kuwepo kwa kutumia bidhaa zake katika mfumo wa kizazi kijacho wa mtandao wa simu wa 5G.

Nchi kadhaa zimeelezea wasiwasi kuwamba bidhaa za Huawei zinaweza kutumika katika uangalizi wa China, tuhuma ambazo hatahivyo kampuni hiyo imezikana vikali.

Huawei imesema shughuli zake sio tishio na kwamba inafanya kazi pasi kuitegemea serikali ya China.

Hatahivyo baadhi ya matiafa zimepiga marufuku makampuni ya mawasiliano kutumia bidhaa za Huawei katika mtandao huo wa 5G.


Mvutano huu una maana gani kwa vita vya kibiashara kati ya Marekani na China?

Hatua hiii ya sasa dhidi ya Huawei inadhihirisha kuongezeka kwa uhasama kati ya kampuni hiyo na serikali ya Marekani.

Kampuni hiyo inakabiliwa na kesi kadhaa za uhaifu zilizowasilishwana maafisa Marekani.

Washington pia inataka mkurugenzi mtendaji wa Huawei ahamishwe kutoka Canada kupelekwa Marekani Meng Wangzou ambako alikamatwa kutokana na ombi la maafisa wa Marekani.

Haya yanajiri wakati uhasama wa kibiashara katiya Marekani na China unaonekana kuongezeka.

Mataifa hayo mawili makuu kibiashara duniani yamekuwa yakizozana kwa mwaka mmoja uliopita iliochangia kuidhinihswa jwa kodi ya mabilioni ya dola ya thamani ya bidhaa za kila upande katika mzozo huo.

Na mzozo huu wa kibiashara umeathiri uchumi duniani katika mwaka uliopita na kufanya kuwepo wasiwasi kwa biashara na wateja.