Aliyekuwa kiongozi wa Tunisia Zine Ben Ali azikwa Saudi Arabia

Nipashe Online: Aliyekuwa kiongozi wa kidikteta nchini Tunisia Zine Ben Ali alizikwa jana Jumamosi uhamishoni nchini Saudi Arabia.

Ben Ali aliyekuwa na umri wa miaka 83, alizikwa katika mji mtakatifu wa Saudi Arabia, Medina .Ben Ali alifariki siku ya Alhamisi katika hospitali moja nchini Saudi Arabia kutokana na ugonjwa ambao haukutajwa .

Wakili wake amesema kuwa familia ya Ben Ali haitarejea nchini mwao kutokana na sababu za kisheria.

Baada ya kung’atuliwa kwake mamlakani, Ben Ali alishtakiwa bila kuwepo kwa makosa mbali mbali yanayohusiana na vifo vya waandamanji na ufisadi.

Ben Ali alikuwa ameiongoza Tunisia kwa muda wa miaka 23 iliyokumbwa na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu.