Jengo la kutengenezea ndege ya Boeing ndilo kiwanda kikubwa zaidi duniani

Kiwanda hicho sasa kinaunda kizazi kipya cha ndege aina ya Boeing

Nipashe Online: Shirika la Boeing lilipoamua kuunda ndege yake chapa 747 – lilijizolea sifa kwa kufungua mlango wa kutengeneza ndege kubwa zaidi duniani.

Hata hivyo shirika hilo lililazimika kujenga kiwanda kikubwa zaidi ambacho kina uwezo wa kukidhi mahitaji ya ndege hiyo.

Ikiwa umewahi kuona ndege aina ya 747 ikiwa karibu, bila shaka utafahamu ukubwa wa ndege hiyo.

Kwa hivyo si ajabu kuona kiwanda kilichounda ndege hiyo kuishia kuwa na jumba kubwa zaidi la kiwanda.

Jengo kubwa kiasi gani?

Boeing ilianza kujenga kiwanda cha Everett mwaka 1967, muda mfupi baada ya mradi wake wa Boeing 747 kuanza kushika kasi.

Bill Allen, mmoja wa viongozi wa ngazi ya juu katika kampuni ya Boeing, anasema shirika hilo lilifahamu fika kuwa, linahitaji sehemu kubwa, endapo lina mpango wa kuunda ndege ya kubeba abiria 400.

Waliamua kuchagua eneo la takriban kilomita 35 Kaskazini mwa jiji la Seattle, karibu na uwanja wa ndege ambao ulitumika kama kituo cha vita wakati wa vita vikuu vya pili vya dunia.

Ripoti katika jarida la Daily Herald liliangazia eneo hilo lililokuwa tu na barabara ndogo mno ya kufikia barabara kuu ya lami, na hakukuwa na njia ya reli kabisa kuunganisha eneo hilo, huku ukizungukwa na msitu ambao ulikuwa makao ya dubu, waliokuwa wakirandaranda humo.

Boeing ililazimika kujenga kiwanda kipya wakati ilipokuwa ikitengeneza muundo wa ndege ya aina ya 747Haki miliki ya picha BOEING-Boeing ililazimika kujenga kiwanda kipya wakati ilipokuwa ikitengeneza muundo wa ndege ya aina ya 747

Wakakati huo huo, Boeing ilikuwa ikijenga mojawepo ya uwanja mkubwa zaidi wa ndege duniani, pia kujenga kiwanda kikubwa zaidi cha kuunda ndege, kuwemo uwanjani humo.

Leo, Kiwanda cha Everett kinapiku jumba lolote lile duniani kwa ukubwa na upana, huku kitabu cha kuandika maswala ya maajabu ya dunia- The Guenness Book of Records, kikiripoti kuwa jumba hilo lina ukuwa wa mita za upana milioni13.3 sawa na futi milioni 472.

“Tulijenga jumba hilo kubwa juu ya baadhi ya maeneo maarufu sana duniani,” anasema David Reese, ambaye alikuwa akisimamia usafiri wote wa utalii wa kampuni ya Everett. “Tuko na maeneo maarufu kama vile Versailles, Vatican na Disneyland, na unayaona mara tu unapoanza ziara ya kuzuru kiwanda chetu.

Jumba kuu la Everett, linakaa juu ya ekari 97.8 ya ardhi, mara ukubwa mra 30 zaidi ya viwanja maarufu vya Trafalgar Jijini London.

“Nakumbuka nikifanya mahojiano na BBC miaka michache iliyopita, na nikajiuliza, ‘hivi uwanja wa Wembley unaukubwa kiasi gani? Naam, jawabu lake ni kuwa uwanja huo unaingia mara 13 ndani ya eneo lote la kiwanda chetu.”

Hadi sasa kampuni ya Everett ingali ikiunda ndege chache za aina ya 747, lakini kwa sasa imejiwekeza zaidi kwenye uundwaji wa aina ndogo za 767, 777 na 787. Hata hivyo, ili kutengeneza ndege hizo, angali eneo kubwa hilo linahitajika.

Ndege zilizo kamilishwa kuundwa huvutwa kwenye daraja hadi karibu na uwanja wa ndege uliyo karibuHaki miliki ya picha BOEING-Ndege zilizo kamilishwa kuundwa huvutwa kwenye daraja hadi karibu na uwanja wa ndege uliyo karibu

Kila zamu ilikuwa na wafanyikazi wengi wapatao elfu 10, na kulikuwa na zamu tatu kwa siku. Katika kipindi cha saa 24 pekee, watu wote wanaofanya kazi katika kampuni hiyo, inazidi jumla ya wakaazi wote wa mji wa Alice Springs nchini Australia.

Reese ameifanyia kazi kampuni ya Boeing jumla ya miaka 38 – miaka 11 kati ya hiyo akisimamia idara ya utalii ya kampuni hiyo- lakini anasema angali anakumbuka taswira ya kwanza aliyoiona alipofika kiwandani hapo kwa mara ya kwanza.”Ilikuwa na mvutio mkubwa mno- na naweza kusema kuwa hali ilikuwa vivyo hivyo kila siku. Hali ilianza kubadilika, kila siku kitu kipya kilitokea.”

Kiwanda cha Everett ni kikubwa mno kiasi cha kuwa na zaidi ya baiskeli 1,300 tayari kusaidia katika kupunguza muda wa usafiri. Kina kituo chake cha zima moto, huduma za matibabu na migahawa chungu nzima ya kuwapa lishe maelfu ya wafanyikazi.

Juu kuna mamia ya kreni inayobeba baadhi ya vipuri vizito vya ndege huku ujenzi wa ndege ukiendelea. Wahudumu, Reese anasema kuwa ni miongoni mwa watu walio na ujuzi mkubwa mno, na ni wafanyikazi wanaolipwa pesa nyingi sana kiwandani.

Wakati wa msimu wa kiangazi, hali huwa na joto jingi, huku milango mikubwa ikifunguliwa, ili kuruhusu upepo mwanana kuingia ndani ya maeneo ya kazi.

Kuna sheria kadhaa za kazi, au hata wakati wa ziara ndani ya kiwanda. “Mtu anafaa kuwa na viatu maalumu, kwani viatu vya wazi au vyenye visigino virefu kwa kina dada haviruhusiwi kabisa- ili kujilinda na majeraha kiwandani. Kuvaa miwani ya usalama ni lazima wakati wote mtu akiwa kiwandani.

Hilo linaweza kuwa kero kidogo miongoni mwa baadhi ya wageni, mara kwa mara wanalalamika- na kusema maneno kama ‘Oh, navalia miwani tu ya kusoma …basi! kwani hiyo haitoshi?”

Kiwanda kinajivunia baadhi ya mapambo. Huku kukiwa na vijidirisha vya kupitishia hewa safi, hakuna kabisa vifaa vya hewa baridi hasa wakati hali ya joto linaongezeka. Wakati wa msimu wa baridi, Athari ya vifaa vingi vya umeme husaidia zaidi ya wafanyikazi 10,000 kupata joto. “Nivalia tu fulana au jaketi nyepesi tu na hiyo yatosha.”

Reese anasema kwamba, “Mara tulipokamilisha kuunda ndege ya kwanza na kisha kuitoa nje ya kiwanda ili kuendeshwa katika uwanja wa ndege ulioko karibu, tulifanya hilo usiku.”

Ama kwa kweli, siyo tu jumba kubwa zaidi duniani, bali pia kuna vitu kadha wa kadha vya kushangaza.